Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete usiku wa leo, Ijumaa, Oktoba 23, 2015, amewateua Makatibu Wakuu wanne wapya wa wizara mbali mbali.
Aidha,
Rais Kikwete amewateua Naibu Makatibu Wakuu wapya watano, amewateua
Makatibu Tawala wa Mikoa wawili na pia amewahamisha Naibu Makatibu Wakuu
wawili.
Kwa
mujibu wa uteuzi huo, Rais Kikwete amemteua Ndugu Hab Mkwizu kuwa
Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma; Profesa
Elisante Ole Gabriel kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana,
Utamaduni na Michezo; Dkt. Yamungu Kayandabila kuwa Katibu Mkuu wa
Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia na Mhandisi Omari Chambo
kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini.
Aidha,
kwa mujibu uteuzi huo, Rais Kikwete amemteua Mhandisi Paul M. Masanja
kuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Nishati na Madini; Dkt. Maria Mashingo
kuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Mifugo na Uvuvi na Ndugu Zidikheri M.
Mundeme kuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika.
Wengine
walioteuliwa kuwa Naibu Makatibu Wakuu ni Ndugu Tixon T. Nzunda ambaye
anakuwa Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa
Umma na Ndugu Emmanuel Kalobelo ambaye anakuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara
ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia.
Walioteuliwa
kuwa Makatibu Tawala wa Mikoa ni Ndugu Eliakim Maswi ambaye anakuwa
Katibu Tawala wa Mkoa wa Manyara na Mhandisi Madeni Kipande ambaye
anakuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Katavi.
Katibu
Mkuu ambaye anahamishwa ni Bibi Sihaba Nkinga ambaye anakwenda kuwa
Katibu Mkuu wa Wizara ya Wanawake, Jinsia na Watoto kutoka Wizara ya
Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo.
Naibu
Makatibu Wakuu wanaohamishwa ni Ndugu John T. Mngodo ambaye
anahamishiwa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kutoka Wizara ya Uchukuzi
na Ndugu Mwamini Juma Malemi ambaye anakwenda kuwa Naibu Katibu Mkuu,
Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo.
Wateuliwa hao wote wataapishwa asubuhi ya kesho, Jumamosi, Oktoba 24, 2015, Ikulu mjini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment