Watu sita wamejeruhuiwa kwa mapanga sehemu mbalimbali za miili yao Wilayani Tarime mkoani Mara akiwemo mwandishi wa habari wa Sahara Media, Geoge Nteminyanda (49) usiku wa kuamkia leo.
Wakizungumza
na mwandishi wa habari wa gazeti la Mwananchi katika wodi namba tatu na
namba nane walikolazwa, majeruhi hao wamesema kuwa walishambuliwa na
wafuasi wa vyama vya Chadema na CCM ambao walikuwa katika makundi
makundi kati ya saa mbili na saa nne usiku.
Nteminyanda
ambaye ni mkazi wa Kisesa Mwanza amesema kuwa aliitwa na mgombea
ubunge wa CCM, Michael Kembaki na kufikia katika hoteli ya CMG ambapo
kulikuwa na kikao cha chama hicho lakini alianza kuhojiwa na baadhi ya
wanachama wa chama hicho. Lakini licha ya kutoa vitambulisho vya kazi
wafuasi hao walianza kumshambulia kwa kumpiga mapanga mwilini na
kuanguka chini. Hata hivyo watu hao waliendelea kumkanyaga hadi
akapoteza fahamu.
Wasamaria wema walimchukua na kumpeleka hospitalini ambapo alipewa kitanda namba tatu cha wodi namba tatu.
“Waliokuwa
wakinishambulia walikuwa vijana wengi kutokana na kunikabiri vibaya
sikuwatambua kwa haraka lakini wakiwekwa kwenye mstari wa utambuzi
nitawatambua” amesema Nteminyanda.
Wengine
waliojeruhiwa ni Waiboga warioba (37) aliyekatwa kichwa na sikio la
kulia,Busiro Rhobi (28) mkazi wa Nyamongo aliyekuwa na gari lake
binafsi, Daniel Mathew (18) mkazi wa Goribe Wilayani Rorya anayedaiwa
kupigwa risasi kichwani upande wa kulia na mgombea udiwani wa kata ya
Ikoma Laurence Andriano (CCM).
Wengine
ni Wambura Marai (38) aliyeopolewa kutoka kwenye gari lake baada ya
kutokea ubishani kati yake na wafuasi wa CHADEMA kuwa mshindi urais
atakuwa John Pombe Magufuli.
Rose
Hosea muuguzi mfawidhi wa Hospitali ya Wilaya Tarime amesema kuwa
wakati wanapokelewa hali yao ilikuwa mbaya zaidi lakini kutokana na
juhudi za timu ya wauguzi wa zamu walitoa huduma za haraka ikiwa ni
pamoja na kuwashona majeraha yao huku wakiwapa dawa za maumivu.
“Hali yao inaendelea vizuri kwa sasa tofauti na ilivyokuwa jana” amesema Hosea.
No comments:
Post a Comment