Kamanda Mkuu wa polisi mkoa Arusha, Liberatus Sabas amesema jeshi hilo limebaini uwepo wa vikundi vilivyojipanga kufanya vurugu na kuvionya kuacha mara moja.
Akizungumza
na waandishi wa habari leo ,amesema mpaka sasa wameweza kubaini zaidi
ya watu 100 wakiwa ni vijana ambao wamesambazwa Arusha mjini pamoja na
wilaya ya Arumeru kwaajili ya kufanya vurugu wakati wa uchaguzi .
Amesema
jeshi la polisi limejipanga kukabiliana na uhalifu au vurugu zozote
zitakazotokea katika kipindi cha uchaguzi kwa kuwa tayari wamepokea
tetesi za kuwepo kwa makundi hayo.
“Natoa
onyo kwa hayo makundi kuwa kama wanataka usalama waache mara moja zoezi
hilo, kwa kuwa hawatakuwa salama ,”amesema Liberatus .
Kamanda
huyo amewataka wakazi wa Arusha kuzipuuzia dhana potofu kuwa polisi
wapo kwa ajili ya kupiga wanachi na kusema kuwa sheria itachukua mkondo
wake kwa watakaofanya vurugu.
“
Kazi ya polisi si kupiga watu ,kazi ya polisi ni kulinda, sisi tunasema
ukipiga kura na uende kwako kama sheria inavyosema ,hakuna kukaa mita
200 ,300 hata 500 ,wote waende nyumbani ,” amesema.
No comments:
Post a Comment