Kimbunga
hicho hata hivyo hakijasababisha uharibifu mkubwa kama ilivyohofiwaRais
wa Mexico ameonya kuwa Kimbunga Patricia bado kinaweza kusababisha
mafuriko na maporomoko ya ardhi huku mvua kubwa iliyotokana na kimbunga
hicho ikiendelea kunyesha maeneo ya taifa hilo.
Rais
Enrique Pena Nieto alisema Patricia, ambacho ndicho kimbuka kikali zaidi
kuwahi kuripotiwa maeneo ya Amerika, kufikia sasa kimesababisha madhara
madogo ikilinganishwa na ilivyotarajiwa.
Kituo cha
kitaifa cha kufuatilia vimbunga cha Marekani (NHC) kilisema kimbunga
hicho kilfikia ngazi ya tano, ambayo ndiyo ya juu zaidi.
Baadaye, kimbunga hicho kilishushwa ngazi na kuwekwa kwenye ngazi ya pili.
Kimbunga hicho kilifika maeneo ya magharibi mwa Mexico na kusababisha upepo mkubwa na mvua, lakini uharibifu mkubwa haukutokea.
Kituo cha NHC kilisema upepo huo ulikuwa umepunguza kasi hadi kilomita 155 kwa saa, kilipokaribia bara.
Kimbunga hicho kwa sasa kinaelekea maeneo ya kaskazini mashariki.
Majimbo ya Nayarit, Jalisco, Colima, Michoacan, na Guerrero ndiyo yaliyo hatarini, kituo hicho kimesema.
"Ripoti
za kwanza za uharibifu zinaonyesha uharibifu uliotokea si mbaya kama
ilivyotarajiwa kwa kimbunga cha ngazi hiyo,” Bw Pena Nieto amesema
akihutubia taifa kupitia runinga.
Kimbunga
hicho kimeandamana na upepo na mvua kubwaPolisi nchini Mexico walisema
visa pekee vilivyoripotiwa ni vya maporomoko madogo ya ardhi na kuanguka
kwa miti.
Lakini
serikali imeonya kuwa majivu kutoka kwa mlima wa Colima, ambao unatoa
moshi, huenda yakachanganyikana na mvua kubwa na kusababisha maporomoko
makubwa ya ardhi.
Watu 400,000 hukaa maeneo yaliyo hatarini, kwa mujibu wa Hazina ya Kitaifa ya Kukabiliana na Majanga ya Mexico.
No comments:
Post a Comment