Taxi zasusia kumbeba msanii mweusi Australia
Msanii
nguli raia wa Australia al maarufu ''Uncle'' amekiri kuwa amebaguliwa
mara nyingi tu hata na madereva wa teksi wanaokataa kumbeba.
Jack
Charles amesema kuwa katika siku tatu zilizopita madereva wa teksi
wamesusia kumbeba mara 2 licha ya umaarufu wake kama 'Uncle'
Meneja
wake Patrice Capogreco, sasa anasema kuwa msanii huyo anatafakari
kuwafungulia mashtaka ya ubaguzi madereva hao wa teksi na kampuni
zilizowaajiri.
Tukio la
kwanza lilitokea usiku wa Jumatano iliyopita mjini Melbourne msanii huyo
Charles alipokuwa akitoka kwenye dhifa aliyotuzwa taji la ''Victorian
Senior Australian of the Year''.
Msanii huyo anatafakari kuwafungulia mashtaka ya ubaguzi
Yamkini alipomsimamisha dereva mmoja wa teksi alidai alipwe kwanza kwani ''alihofia msanii huyo hakuwa na pesa za kulipa''
Na hata
kabla hajasahau tukio hilo la kibaguzi, 'uncle' kama anavyofahamika,
alisimamisha teksi nyengine impeleke kwenye uwanja wa ndege wa Melbourne
ijumaa.
'uncle' aliachwa ameduwaa dereva mwengine wa taksi alipovurumisha gari lake na kutoweka.
Halmashauri inayosimamia utoaji leseni katika mji huo tayari umeanzisha uchunguzi kuhusiana na matukio hayo.
Msemaji wake ameiambia BBC kuwa halmashauri hiyo haitavumilia ubaguzi wa aina yeyote.
Halmashauri inayosimamia utoaji leseni katika mji huo tayari umeanzisha uchunguzi kuhusiana na matukio hayo.
Halmashauri
hiyo ilionya kuwa ''madereva wa teksi sharti wawe tayari kumhudumia
mgeni yeyote bila kumbagua kwa misingi ya rangi ,tabia ama jinsia''
''Nauli ya teksi kuanzia saa nne usiku sharti ilipwe na mteja kabla hajabebwa kuanzia saa nne hadi saa kumi na moja asubuhi.
''Uncle'' ameiambia BBC kuwa sio tukio la ajabu miongoni mwa wa-Australia wa asili.
Mara nyingi wa-Australia wa asili hulazimika kuomba msaada wa wageni kuwasimamishia teksi.
No comments:
Post a Comment