Highness Kiwia akionyesha moja ya karatasi yenye makosa
Na:George Binagi-GB Pazzo
Aliekuwa
Mbunge wa Jimbo la Ilemela Mkoani Mwanza na Mgombea wa nafasi hiyo
kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema chini ya mwamvuli wa
Umoja wa Katiba ya Wananchi Ukawa Highness Kiwia, anatarajia kufungua
kesia ya kupinga matokeo ya uchaguzi jimboni humo kwa madai kwamba
haukuwa wa huru na haki kutokana na kugubikwa na changamoto mbalimbali.
Kiwia
ambae ameshindwa kutetea jimbo hilo baada kuchukuliwa na Angelina
Mabula kutoka Chama cha Mapinduzi CCM, aliyasema hayo jana wakati
akizungumza na wanahabari kuhusiana na Uchaguzi huo.
Alieleza
kuwa katika vituo mbalimbali jimboni humo kulikuwa na makosa mengi
ambayo ni pamoja na uwepo wa vituo hewa, idadi ya wapiga kura
kutofautiana na idadi ya waliojiandikisha katika daftari la kupigia kura
pamoja na majina ya wapiga kura kukutwa katika majimbo tofauti na yale
waliyojiandikishia.
Katika
hatua nyingine Kiwia alikanusha taarifa kuwa alimtuma mwakilishi kwa
ajili ya kusaini fomu ya matokeo kwa niaba yake na kwamba siku ya
kutangaza matokeo alishindwa kupokea matokeo hayo na hivyo kuzilai.
Kwa
upande wake Tungaraza Njugu ambae ni Kiongozi wa Kanda ya Ziwa Victoria
Chadema, alisema kuwa zoezi la uchaguzi mwaka huu linapaswa kulaaniwa
kwa kuwa halikuendeshwa kidemokrasia kutokana na kukiuka taratibu
mbalimbali za uchaguzi.
Katika
Matokeo ya Kiti cha Ubunge Jimboni Ilemela, Mgombea wa CCM Angelina
Mabula aliibuka mshindi baada ya kupata kura 85,424 na kufuatiwa na
mgombea wa Chadema Highness Kiwia aliepata kura 61,679 ambapo kwa upande
wa Madiwani CCM ilishinda Kata 16 huku Kata Tatu zikichukuliwa na
upinzani.
BONYEZA PLAY HAPA CHINI KUSIKILIZA
Aliekuwa Mbunge wa Jimbo la Ilemela Mkoani Mwanza na Mgombea wa nafasi hiyo kupitia Chadema.(P.T)
Aliekuwa Mbunge wa Jimbo la Ilemela Mkoani Mwanza na Mgombea wa nafasi hiyo kupitia Chadema akiongea na wanahabari
Kiwia akiteta jambo katika Mkutano na Wanahabari
Kutoka
Kushoto ni Humphrey Mhada ambae ni Mwenyekiti Kanda ya Ziwa Victoria
Chadema, Highness Kiwia ambae alikuwa mgombea Jimbo la Ilemela Chadema
na Hassan Haji ambae alikuwa Meneja Kampeni Jimboni Ilemela
Press Conference
Aliekuwa Mbunge wa Jimbo la Ilemela Mkoani Mwanza na Mgombea wa nafasi hiyo kupitia Chadema akiongea na wanahabari
Wa kwanza
kulia waliokaa ni Tungaraza Njugu ambae ni Kiongozi wa Kanda ya Ziwa
Victoria Chadema akiongea katika mkutano na wanahabari
Peter Kaiza ambae alikuwa Mgombea Udiwani Kata ya Ibungilo Ilemela akionyesha moja ya karatasi yenye makosa
Kutoka
Kushoto ni Julius Malifedha ambae ni Katibu Mwenezi Chadema Ilemela,
Peter Kaiza aliekuwa Mgombea Udiwani Kata ya Ibungilo na Ivonne Highness
ambae alikuwa Mratibu wa Kampeni za Uchaguzi
Kada wa Chama
No comments:
Post a Comment