Marekani
imeiondoa Burundi kutoka kwenye mikataba yake ya kibiashara AGOA
iliyowezesha mataifa ya Afrika kuingiza bidhaa zao katika soko la
Marekani bila kulipa kodi.
Katika
barua aliyoiandikia bunge la Congress , rais Barrack Obama ameelezea
kuwa amechukua hatua hiyo baada ya kushuhudia kushuka kwa viwango vya
demokrasia katika taifa hilo la Afrika ya Kati.
''Burundi
haijafanya jitihada zozote za kurejesha amani na utangamano''
Obama.''Burundi haijafanya jitihada zozote za kurejesha amani na
utangamano'' Obama.
Obama
alisema kuwa badala ya kuimarika kidemokrasia, Burundi inaendelea
kushuhudia wapiganiaji wa haki za kidemokrasia wakikamatwa na kufungwa
jela huku wengine wengi wakiuawa kwa kudai haki zao za kikatiba
zifwatwe.
Aidha
Obama ameelezea kuwa hatua ya serikali ya rais Nkurunziza ya
kuwanyamazisha makundi ya wapinzani kwa kuwashika kuwaua na hata
kuwatesa ni kinyume na maadili ya taifa linalodai kuzingatia demokrasia.
Takriban
watu 200 wameuaawa tangu machafuko yaanze mwezi ApriliMarufuku hiyo ya
Burundi inaanza kutekelezwa mwezi januari mwakani.
Burundi
ilitumbukia katika mzozo wa kisiasa na kukumbwa na machafuko punde baada
ya rais Pierre Nkurunziza kutangaza nia ya kuwania muhula wa tatu
kinyume na katiba ya taifa.
Aidha kulitokea jaribio la mapinduzi lakini likazimwa.
Takriban
watu 200 wameuaawa tangu machafuko yaanze mwezi Aprili upinzani
ulipopinga hatua ya Nkurunziza kushiriki kwenye uchaguzi kwa muhula wa
tatu.Nkurunziza alishiriki uchaguzi huo na akashinda, hata hivyo
kumeendelea kuwa na visa vya maandamano,mauaji na kutoweka kwa wapinzani
wake.
Takriban watu 200 wameuaawa tangu machafuko yaanze mwezi Aprili
Inakisiwa kuwa watu 200,000 wametoroka makwao na sasa wanaishi kwenye kambi za wakimbizi katika mataifa jirani.
Mpango wa
AGOA (African Growth and Opportunity Act) ulianzishwa yapata muongo
mmoja uliopita ilikuzisaidia mataifa maskini ya Afrika kuuza bidhaa zao
katika soko la Marekani.BBC
No comments:
Post a Comment