Jeshi
la Polisi Zanzibar kwa kushirikiana na Jeshi la Wananchi (JWTZ),
limefanikiwa kuteguwa bomu lilitegwa eneo la Mkunazini karibu na kituo
cha polisi mjini Zanzibar.
Bomu
hilo lilitegwa na watu wasiofahamika na jeshi la polisi lilipata
taarifa ya kutegwa kwa bomu hilo kutoka kwa wasamaria wema.
Akizungumza
na mwandishi wetu, Kamishna wa Jeshi la Polisi Zanzibar, Hamdani Omar
Makame, alisema baada ya kupata taarifa kutoka kwa wananchi kuwa eneo
hilo kuna kitu kimetegeshwa, jeshi la polisi lilifanya uchunguzi na
kubaini kuwa ni bomu na kufanikiwa kulitegua kwa kuliripua ili kuepusha
maafa.
“Ni kweli kulikuwa na kishindo kikubwa baada ya jeshi la polisi kuliripua bomu hilo lakini hakuna madhara yoyote yaliotokea,” alisema.
Aidha
alisema kuwa jeshi la polisi linaendelea na uchunguzi ili kubaini ni
aina gani ya bomu lililotegwa na aliyefanya kitendo hicho.
No comments:
Post a Comment