Mji wa
Bagamoyo zamani ulitumiwa kuwazuilia watumwa kabla yao kupelekwa
ZanzibarUjenzi wa bandari inayotazamiwa kuwa kubwa zaidi katika kanda ya
afrika mashariki umeanza nchini tanzania.
Bandari
hiyo inayojengwa katika mji wa bagamoyo itakuwa na uwezo wa kukimu
mashehena milioni 20 kila mwaka, idadi ambayo ni mara mbili zaidi ya
bandari inayotumika sasa jijini Dar es Saalam.
Mradi huo utagharimu takriban dola bilioni 11, huku ufadhili mkubwa wa kiasi hicho ukitoka nchini china.
Serikali ya Tanzania inasema kuwa mradi huo utaiwezesha kushindana na Kenya katika biashara za kikanda na rubaa za kimataifa.
Bandari hiyo inatarajiwa kutoa ushindani mkali kwa bandari iliyo mjini Mombasa katika taifa jirani la Kenya.
Mji wa
Bagamoyo umo kilomita 75 kaskazini mwa Dar es Salaam na ndilo eneo
anamotoka Rais Jakaya Kikwete anayeondoka mamlakani baada ya uchaguzi wa
urais Oktoba 25.
Bagamoyo
ulikuwa ndio mji mkuu wa awali wa kikoloni chini ya Wajerumani na
ulikuwa kituo kikuu katika biashara ya utumwa. Watumwa waliwekwa katika
mji huo kwa muda kabla ya kusafirishwa hadi soko kuu katika kisiwa cha
Zanzibar.
No comments:
Post a Comment