Waandishi wa Habari mkoani Mbeya wakiwa ndani ya Pango katika maporomoko ya Kaporogwe ambapo sehemu hiyo haiguswi na maji ya mvua ikinyesha.
Mwishoni
mwa wiki, wanahabari mkoani Mbeya kupitia chama chao cha Mbeya Press
Club (MBPC) walitembelea maporomoko ya maji ya Kapologwe yaliyopo katika
kijiji cha Bugoba kata ya Kisondela.
Wanahabari
walifika kwenye maporomoko hayo ikiwa ni sehemu ya ziara yao ya
kimafunzo waliyoifanya katika vijiji mbalimbali vya kata ya Kisondelo
lengo likiwa ni kujifunza juu ya maisha ya wakazi wa vijiji hivyo.
Mwenyekiti
wa chama cha waandishi wa habari mkoa wa Mbeya (MBPC) Modestus Nkulu
alisema:“Maporomoko kama haya ni hazina tosha kiutalii. Wengi wetu
hatukuwahi amini kuwa ipo siku tutakutana na mambo ya ajabu kama haya.
Uwepo wa
pango kubwa kama tuliloliona na pia maji yanayotiririka hapa ni mambo ya
ajabu sana. Nawasihi Watanzania wengine tuimarishe utalii wa ndani kwa
kutembelea kivutio hiki” alisisitiza Nkulu.
Wanahabari wa Mkoa wa Mbeya wakichukua kumbukumbu mbali mbali katika
maporomoko ya Kapologwe yaliyoko Wilaya ya Rungwe mkoani Mbeya.
Wanahabari wa Mkoa wa Mbeya wakichukua kumbukumbu mbali mbali katika maporomoko ya Kaporogwe yaliyoko Wilaya ya Rungwe mkoani Mbeya. |
Wanahabari wa Mkoa wa Mbeya wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya kushuka kwenye maporomoko ya Kaporogwe. |
Wanahabari wa Mkoa wa Mbeya wakielekea sehemu ya Maporomoko |
Waandishi wa Habari mkoani Mbeya wakiwa ndani ya Pango katika maporomoko ya Kaporogwe ambapo sehemu hiyo haiguswi na maji ya mvua ikinyesha. |
Baadhi ya wanahabari wakipunzika katika mapango yaliyoko katika maporomoko ya Kaporogwe |
Kumbukumbu mbali mbali zikichukuliwa |
Wanahabari wakiendelea kuhojiana baada ya kuridhika na kile walichokiona katika ziara yao. |
WANANCHI wametakiwa kujitokeza kujifunza kutokana na maeneo ya vivutio vya utalii vilivyopo katika maeneo yao ili kukuza uchumi wa ndani.
Hayo yalibainishwa mwishoni mwa wiki na Wanahabari mkoani Mbeya kupitia chama chao cha Mbeya Press Club(MBPC) walipotembelea maporomoko ya maji ya Kapologwe yaliyopo katika kijiji cha Bugoba kata ya Kisondela wilayani hapa.
Wanahabari walifika kwenye maporomoko hayo ikiwa ni sehemu ya ziara yao ya kimafunzo waliyoifanya katika vijiji mbalimbali vya kata ya Kisondelo lengo likiwa ni kujifunza juu ya maisha ya wakazi wa vijiji hivyo.
Wakizungumza mara baada ya kutembelea maporomoko ya Kaporogwe,wanahabari waliokuwa kwenye ziara hiyo walisema maporomoko hayo ni moja ya vivutio vya utalii vinavyopaswa kutangazwa zaidi ili kuwezesha watu kutoka ndani na nje ya nchi kuyatambua.
Mwenyekiti wa chama cha waandishi wa habari mkoa wa Mbeya(MBPC) Modestus Nkulu alisema maporomoko hayo ni miongoni mwa hazina zenye manufaa makubwa iwapo zitatangazwa na kuhamasisha jamii kuyatambelea.
“Maporomoko kama haya ni hazina tosha kiutalii.Wengi wetu hatukuwahi amini kuwa ipo siku tutakutana na mambo ya ajabu kama haya.Uwepo wa pango kubwa kama tuliloliona na pia maji yanayotiririka hapa ni mambo ya ajabu sana.Nawasihi watanzania wengine tuimarishe utalii wa ndani kwa kutembelea kivutio hiki” alisisitiza Nkulu.
Alisema kwa wakazi waishio mkoani Mbeya hawapaswi kusimuliwa juu ya uwepo wa maporomoko haya ya ajabu mkoani kwao hivyo wana fursa nzuri ya kufika na kujionea ili wanaposafiri kwenda mikoa mingine wakiulizwa na wenzao huko wawe na majibu sahihi.
Nao wanahabari Joachim Nyambo na Amina Said walisema ziara hiyo imekuwa na mafanikio makubwa kimafunzo kutokana na mambo waliyoyashuhudia wakisema hiyo itakuwa chanchu ya kutangazwa kwa vivutio vya utalii.
Walishauri wadau mbalimbali mkoani hapa kuona umuhimu wa kuwawezesha wanahabari kuvifikia vivutio vya utalii vilivyopo ndani ya mkoa wao.
No comments:
Post a Comment