Na RFI
Zaidi ya watu 30 wameuawa baada ya kutokea kwa milipuko mitatu ya kujitoa mhanga mjini Maiduguri Kaskazini mwa nchi ya Nigeria.
Ripoti
zinasema kuwa mashambulizi hayo yalitekelezwa na wasichana watatu
wanaoaminiwa kuwa kati ya miaka 11 na 15 mapema siku ya Ijumaa.
Shirika
la kushughulikia majanga ya dharura linasema shughuli za kutafuta miili
zaidi linaendelea pamoja na kuwapa hudumu za matibabu wale
waliojeruhiwa.
Shambulizi
hili la Ijumaa linakuja baada ya kutokea kwa shambulizi lingine kama
hili siku ya Alhamisi lililosababisha vifo vya watu 32 katika mji huo wa
Maiduguri.
Shambulizi la jana liliwalenga Waislamu waliokuwa wanaswali sala ya jioni na pia kusabibabisha majeraha.
Kundi la
Boko Haram halijajitokeza kudai kutekeleza mashambulizi haya lakini
maafisa wa usalama nchini humo wameendelea kulishuku.
Mwezi mmoja uliopita zaidi ya watu 100 wamepoteza maisha baada ya kutokea kwa mashambulizi kama haya ya kujitoa mhanga.
Kundi la
Boko Haram limekuwa likitekeleza mashambulizi ya kigaidi kama haya tangu
mwaka 2009 na serikali ya rais Muhamadu Buhari inasema inalenga
kulitokomeza kudni hilo kufikia mwisho wa mwezi Novemba.
No comments:
Post a Comment