Kocha msaidizi wa Yanga Juma Mwambusi (kushto) akiwa sambamba na kocha mkuu wa timu hiyo Hans van der Pluijm
Msimu wa
mwaka 2003-04 kocha Mholanzi Martin Jol alikataa ofa ya kuwa msaidizi wa
Sir Alex Ferguson Manchester United na badala take kuendelea kuwa kocha
mkuu wa klabu ya RCK Waalwijk ya Uholanzi.
Baada ya
kuondokewa na msaidizi wake mreno Carlos Quiroz aliyehamia Real Madrid
wakati huo, Martin Jol alikataa ofa ya kumsaidia Ferguson Manchester
United.
Hali kama
hiyo imetokea nyumbani Tanzania, ambapo baada ya kocha Charles Boniface
Mkwasa kutakiwa na timu ya taifa, klabu ya Yanga ikamhitaji Mwambusi
kuwa msaidizi wao kuziba nafasi iliyoachwa wazi na Mkwasa.
Tofauti
na mholanzi Martin Jol, kocha Juma Mwambusi hakupepesa macho kujiunga na
Yanga kuwa msaidizi hali akiacha nafasi ya ukocha mkuu wa Mbeya City.
Mjadala
umekuwa ni mkubwa kwa wadau wa michezo nchini wakijaribu kuhoji usahihi
wa Mwambusi kuhusiana na kuacha u-boss wa Mbeya City na kuwa msaidizi wa
kocha mkuu wa Yanga.
Kuna kitu
lazima tuwekane sawa hapa; mfumo wa soka letu ni tofauti kabisa na soka
la barani Ulaya. Katika ligi yetu, na hali ilivyo halisi, hakuna uwiano
kati ya vilabu kongwe nchini vya Simba na Yanga na vilabu vingine, Azam
pekee.
Tofauti
ya kimfumo kati ya ligi yetu na ligi zilizoendelea duniani ndiyo kitu
kinachonifanya niamini kuwa Mwambusi yuko sahihi kwa maana ya kwamba
kalamba dume ama galasa.
Hakuna
tofauti kubwa ya kimaslai, wala fursa baina ya timu barani Ulaya na ndio
maana klabu ndogo kamba Wimbledon ina mashabiki wake na wanapata fursa
sawa na klabu nyingine yeyote.
Kwa
Tanzania, tuende mbele turudi nyuma bado ufalme wa klabu za Simba na
Yanga katika soka letu ni mkubwa sana. Ni ngumu sio tu kwa makocha, bali
hata wachezaji kuzikatalia timu hizo zinapowataka.
Ili
uonekane na upate changamoto na exposure ya kutosha kwa nchi yetu,
lazima upitie Simba na Yanga, achilia mbali Azam ambao hivi sasa
wamekamilika na kuzifikia klabu hizo ingawa bado linapokuja suala la
ushabiki, bado Simba na Yanga ni wafalme wa soka ya bongo.
Kiuhalisia,
kutoka Mbeya City kwa Mwambusi na kujiunga na Yanga ni hatua muhimu
katika historia ya career take ya soka. Mwambusi sasa atafahamika,
ataongeza ujuzi na kupata uzoefu wa kutosha kutokana na changamoto
zilizopo katika klabu hizi kubwa tofauti na Mbeya City.
Bila
shaka fursa aliyoipata kocha Boniface Mkwasa kuwa meneja wa timu ya
taifa, imetokana na kiasi kikubwa uwezo na uzoefu alioupata akiwa kocha
msaidizi wa Yanga.
Kesho hatujui nini kiko mbele ya Mwambusi kama ambavyo hatukujua kilichokua mbele ya Mkwasa.
Ingawa
sitaki kuzungumzia masuala ya maslai ‘mtonyo’ ambao Mwambusi atanufaika
zaidi akiwa Yanga tofauti na ilivyokua City, lakini hicho pia sio kitu
cha kubeza hasa kwa maisha yetu ya kiswahili.
Profile
ya Mwambusi sasa imeongeza kitu na kwamba inampa mwanya wa kuwa na fursa
nyingi kubwa mbele yake kama ilivyomtokea Boniface Mkwasa ambaye sasa
ni boss wa timu ya soka ya taifa ya kandanda ya Tanzania.
Mwisho
nitumie fursa hii kumtakia kila la kheri mrithi was Mwambusi Mbeya City.
Kuondoka kwa Mwambusi ni fursa kwake na kwamba ni wakati wa yeye pia
kutengeneza jina lake katika ramani ya soka.
No comments:
Post a Comment