Mamia ya wahamiaji
wamekuwa wakivuka mpaka na kuingia nchini Slovenia wakitokea Croatia,
baada ya Hungary kuwanyima nafasi ya kuingia nchini humo ilipofunga
mipaka yake usiku wa manane.
Serikali ya Slovenia imewahakikishia
wahamiaji hao kuwa safari yao itaendelea vyema hadi wafike Austria, huku
mipaka yao ikisalia wazi.Waziri mkuu wa taifa hilo amesema kuwa wakimbizi walioko huko wanafaa kuhamishiwa kwingine ili kuwe na mpangilio muafaka na salama.
Idadi kama hiyo ya wakimbizi ndiyo iliyowasili nchini Slovenia Jumamosi.


No comments:
Post a Comment