Matokeo ya duru ya
kwanza ya uchaguzi wa urais nchini Guinea yanaonyesha kuwa rais wa sasa
Alpha Conde ameshinda kura za kutosha kuzuia kuwepo duru ya pili ya
uchaguzi.
Huku asilimia 90 ya kura zikiwa zimehesabiwa tume ya
uchaguzi ya nchi hiyo inasema kuwa bwana Conde yuko mbele ya mshindani
wake mkuu Cellou Dalein Diallo.Uchaguzi huo ulifanyika licha ya janga la hivi majuzi la ugonjwa wa ebola ambalo liliwaua maelfu ya watu.


No comments:
Post a Comment