Baadhi
ya raia wa nchini Burundi walioingia nchini kinyume cha sheria wakiwa
kwenye ofisi za idara ya Uhamiaji Mkoa wa Singida wakisubiri kurudishwa
kwao wakiwa chini ya ulinzi wa askari wa kikosi cha uhamiaji
[SINGIDA] Idara
ya Uhamiaji Mkoa wa Singida inawashikilia watu saba raia wa nchini
Burundi waliokutwa wakiwa katika Mji mdogo wa Itigi,wilayani Manyoni kwa
tuhuma za kuingia nchini kinyume cha sheria.
Afisa
uhamiaji Msaidizi wa Mkoa wa Singida,Moses Mandago alisema watu hao
raia wa nchini Burundi walikamatwa okt,saba,mwaka huu,baada ya idara
hiyo kupata taarifa kutoka kwa raia wema za kuwepo kwa raia hao kwenye
eneo la mji mdogo wa Itigi.
Aidha
Mandago alifafanua kwamba madhumuni ya raia hao kutoka nchini Burundi
lilikuwa kwenda Morogoro kufanya biashara,na kumtaja Amani Michael
Horombile (18) kuwa ndiye aliyekwenda mpaka Burundi kuwafuata baada ya
kutumwa na kaka yake aliyetambulika kwa jina la Medsoni Emanueli.
“Lakini
hata hivyo walidai kwamba kuna mtu ambaye anaitwa Amani Michael
Horombile (18),kati ya watu hao saba ndiye aliyeenda mpaka Burundi akiwa
ametumwa na kaka yake anaitwa Medsoni Emanueli ambaye anadai alikuwa
anakaa Turiani,Morogoro”alisisitiza afisa huyo.
Kwa
mujibu wa kaimu afisa uhamiaji huyo waliokamatwa kwa tuhuma za kuvunja
sheria ya nchi ni pamoja na Alex Nintunze (15),Ibrahimu Leopold
(25),Kubwimana Erike(21),Ibrahimu Jafar(17),Hakizimana Yoshuwa(
(13),Kelvin Maliyamungu (14) na Amani Michael Horombile (18).
Watu
hao kwa mujibu wa Mandago walitumia usafiri wa gari moshi kutoka Kigoma
na walikuwa na tiketi zinazoonyesha wanakwenda Tabora lakini walipofika
Itigi,ndipo TT wa gari la moshi aliwashitukia na baada ya kuwahoji
walidai wanakwenda Dodoma na ndipo TT alipowashusha na kuwakabidhi kituo
kidogo cha polisi Itigi.
Hata
hivyo kaimu afisa uhamiaji huyo aliweka bayana kuwa walipofanya
mawasiliano,ikabidi wamtoe afisa mmoja wa idara hiyo hadi Morogoro kwa
lengo la kuutafuta mtandao unaojihusisha na kazi hiyo ya kuwasafirisha
raia hao ili waweze kuusambaratisha.
“Kwa
kushirikiana na maafisa uhamiaji wa Mkoa wa Morogoro wakasema yupo
Dar-es-Salaam na hivyo ndipo afisa huyo aliondoka Morogoro kwenda
Dar-es-Salaam,nia ikiwa ni kumkamata mtuhumiwa huyo ili aweze
kutuonyesha watu hao ili tuweze kujua mtandao huo upo wapi”alisema.
Kutokana
na raia hao kutokuwa na vibali vya kuwaruhusu kuingia nchini,hivyo
idara ya uhamiaji Mkoa wa Singida imechukua hatua za kuwafukuza nchini
kwa kuwasindikiza hadi Mkoani Kigoma .
Hata
hivyo aliweka bayana kuwa matukio kama hayo katika kipindi cha mwaka
2014 hayakuwa ya kutisha sana kutokana na baadhi ya watu kutoka nchini
Ethipia wanaoletwa na kutelekezwa na wenyeji wao kwenye magari.
Akizungumza
kwa niaba ya wahamiaji hao,mmoja wa raia hao wa Burundi,Kelvin
Maliyamungu alikiri kuwa wametokea nchini Burundi na walikuwa
wakisafirishwa kwenda Mkoani Morogoro kufanyakazi ambayo hata hivyo
hakuweza kuifahamu mpaka wakati huo.
Wahamiaji hao wa Burundi..
jengo la Uhamiaji mkoa wa Singida..
No comments:
Post a Comment