Wakili Imelda – Lulu Urio Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa LHRC.
Na Mwandishi wetu
Mtandao
wa Asasi za Kiraia za Kuangalia chaguzi nchini jana ulipata pigo katika
mwendelezo wake wa kukusanya taarifa juu ya mchakato wa uchaguzi mkuu
wa 2015 kama unavyoendelea nchi nzima baada ya Jeshi la Polisi kuvamia
kituo cha kukusanya taarifa kilichopo katika ofisi za Kituo cha Sheria
na Haki za Binadamu ofisi ya Mbezi Beach.
Tukio
hilo lisilo la kawaida lilitokea Majira ya saa nane mchana baada ya
polisi kufika kituoni hapo na kuwaweka wahusika wa kituo hicho wapatao
36 chini ya ulinzi na kuwashinikiza kusimamisha kazi na Kufungua mitambo
bila kutoa sababu ya kufanya hivyo.
Akizungumza
na waandishi wa habari Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa LHRC ambao ndio
waratibu wa TACCEO Wakili Imelda – Lulu Urio amelaani vikali kitendo cha
jeshi la polisi kuvamia na kusimamisha shughuli ambazo zinafanyika kwa
mujibu wa sheria na pia zinafanyika kwa kibali kutoka Tume ya Uchaguzi
ya Tanzania.”
Kitendo
hiki ni cha kidhalilishaji ukizingatia sisi ( TACCEO) tunafanya kazi
kwa mujibu wa sheria na pia tuna vibali vya kufuatilia uchaguzi kwa
mujibu wa sheria” Kituo chetu kinaaminika kwa kufanya kazi kwa maslahi
ya umma wa Tanzania na hii sio mara ya kwanza kwa sisi kufuatilia
uchaguzi za nchi hii hivyo tumeshangazwa na kusikitishwa na kitendo hiki
cha polisi kuvamia bila taarifa” – Aliongeza.
Mkurugenzi
wa Utetezi na Maboresho wa LHRC Wakili Harold Sungusia akizungumza kwa
masikitiko katika eneo la tukio alisema “mpaka sasa hatujui kosa kwani
tumekuwa tukifuatilia chaguzi mbali mbali toka kuanza kwa mfumo wa vyama
vingi nchini na tumekuwa tukifuata sheria na taratibu zote zinazopaswa
kama waangalizi na hata Tume ya Taifa ya Uchaguzi imetupa vitambulisho
vya uangalizi kwa kutambua mchango na nafasi yetu”.
Hata
hivyo sakata hilo bado linaendelea kwani wafanyakazi pamoja na vifaa
vyao vya kazi ikiwemo kompyuta 27 pamoja na simu zao za mkononi ambavyo
vimeshikiliwa na Jeshi la polisi likiongozwa na afisa mpelelezi wa Kituo
cha Polisi cha Kawe aliyefahamika kwa jina la Mgonja. Wafanyakaizi
wamefikishwa Makao Makuu ya Polisi jijini Dar es Salaam kwa uchunguzi
zaidi.
No comments:
Post a Comment