Balozi
Dora Msechu amekutana na watanzania wanaoishi kwenye Jimbo la Fyn
nchini Denmark na kuwapongeza kwa kutimiza miaka 10 ya Umoja wao. na
kuwashukuru kwa mchango mkubwa wanaotoa kwenye maendeleo ya nchi yetu.
Amewaasa waendeleze mshikamano wao na kuwahakikishia kuwa milango ya
Ubalozi ipo wazi katika kuwahudumia na kushirikiana kwa karibu na
watanzania wote wanaoishi kwenye nchi za Nordic na Baltic.
Sherehe hiyo iliandaliwa
na Jumuiya ya Watanzania Jimbo la Fyn kwa kushirikiana na familia ya
Bibi Dorthe Nielsen, rafiki mkubwa wa Tanzania na mtoto wa aliyekuwa
Mwakilishi wa Heshima wa Tanzania nchini Denmark, marehemu
Robert Anderson.
No comments:
Post a Comment