Mratbu
wa shirika la Uwezo mkoa wa Singida, Nason W.Nason, akitoa nasaha zake
kwenye mafunzo yaliyohusu kufanywa kwa utafiti juu ya taaluma shule za
msingi manispaa ya Singida.Wa pili kulia ni Kaimu Afisa Elimu shule za
msingi manispaa ya Singida, Samwel Mwaikenda na (wa pili kushoto) ni
Mkurugenzi wa YMC mkoa wa Singida, Fidelis Yunde.
Kaimu
Afisa Elimu manispaa ya Singida, Samwel Mwaikenda, akizungumza kwenye
ufungaji wa mafunzo ya namna bora ya kufanya utafiti wa taaluma katika
shule za msingi manispaa ya Singida.Wa pili kushoto ni Mkurugenzi wa
shirika la YMC mkoa wa Singida, Fidelis Yunde.
Kaimu
Afisa Elimu shule za msingi manispaa ya Singida, Samwel Mwaikenda,
akimkabidhi kijana Juma cheti kwa kuhitimu mafunzo juu ya utafiti wa
taaluma katika shule za msingi manispaa ya Singida. Mkurugenzi wa
shirika la YMC mkoani Singida, Fidelis Yunde (suti nyeusi) na wa kwanza
kulia, ni Mratibu wa shirika la Uwezo Nason W.Nason.
Baadhi ya
vijana waliohudhuria mafunzo ya siku mbili yaliyohusu kufanya utafiti
juu ya taaluma katika shule za msingi manispaa ya Singida,wakisikiliza
ufungaji wa mafunzo hayo.(Picha na Nathaniel Limu).
Na Nathaniel Limu, Singida
HALMASHAURI
ya manispaa ya Singida, imeahidi kuendelea kushirikiana kwa karibu na
mashirika yasiyo ya kiserikali (NGOs) na wadau wengine wa maendeleo
katika kuboresha sekta mbalimbali,ikiwemo ya elimu.
Ahadi
hiyo imetolewa na Kaimu Afisa Elimu shule za msingi manispaa ya
Singida, Samwel Mwaikenda,wakati akifunga mafunzo ya siku mbili
yaliyohusu utafiti wa taaluma kwenye shule za msingi katika manispaa
hiyo.
Alisema NGos na wadau mbalimbali wamekuwa na mchango mkubwa ambao umesaidia manispaa ya Singida kupiga hatua kubwa ya maendeleo.
“Sina
uhakika lakini nadhani pengine bila haya mashirika na wadau
wengine,manispaa yetu isingekuwa na maendeleo haya makubwa
tunayojuvunia hivi sasa”,alisema.
Kuhusu mafunzo hayo ya utafiti, Mwaikenda amewataka walengwa wa mafunzo hayo wakafanye utafiti ulioshiba ukweli na uhalisia.
“Niwapongeze
YMC kwa kuandaa mafunzo haya muhimu ya utafiti wa hali halisi ya
taaluma ya elimu kwa wanafunzi wenye umri wa kati ya miaka saba na 16.Ni
matarajio yetu kwamba utafiti mtakaoufanya,panoja na mambo
mengine,utasaidia sana kuboresha taaluma kwenye shule zetu za
msingi”,alifafanua kaimu afisa elimu huyo.
Awali
Mkurugenzi wa shirika la YMC mkoa wa Singida.Ferdelius Yunde,alisema
madhumuni na malengo ya mafunzo hayo,ni kuwajengea uwezo vijana 60 wa
kuweza kufanya utafiti juu taaluma kwa watoto wenye umri wa miaka saba
hadi 16.
Akifafanua,
Yunde alisema kuwa vijana hao watafanya utafiti huo kwa kuzingatia
uwezo wa kusoma mtoto,lishe pamoja na mambo mengine watakayoelekezwa,
ili waweze kutekeleza kwa ufanisi mkubwa kazi hiyo muhimu.
“Nitumie
nafasi hii kuwahimiza kwamba nendeni mkaifanye kazi hii kwa uaminifu
mkubwa.Fanyeni tafiti kama mlivyoelekezwa mkizingatia ukweli,endapo
panakuwa na changamoto zilizo nje ya uwezo wenu,toeni taarifa na
tutasaidia kupata ufumbuzi wa kudumu”,alifafanua zaidi Yunde.
Aidha,
amewataka watambue kwamba utafiti wao utasaidia serikali na wadau
wengine kutambua mapungufu yaliyopo katika shule za msingi,na hivyo
kuyatafutia majawabu sahihi.
Kwa
upande wake Mratibu wa shirika la Uwezo, lililopo chini ya shirika la
Twaweza, Nason W.Nason,alisema tafiti hizo zitasaidia kushindanisha
shule za msngi hapa nchini na pia katika nchi za Afrika mashariki, huku
lengo kubwa likiwa na kuboresha talaama kwenye shule za msingi.
Kwa
mujibu wa mkurugenzi Yunde,mafunzo hayo yameratibiwa shirika la YMC na
kufadhiliwa na shirika la Uwezo lililo chini ya shirika la Twaweza.
No comments:
Post a Comment