Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imesema kuwa mashine za kuandisha kwa njia za kielekroniki zilizokamatwa katika kiwanda cha MM Steel, Mwenge, jijini Dar es Salaam sio mashine za BVR kama ilivyodaiwa awali.
Mkurugenzi
wa NEC, Ramadhani Kailima amesema kuwa baada ya kuzifanyia uchunguzi
mashine hizo, wamebaini kuwa mashine hizo ni ‘feki’ na hazifanani na
mashine zilizotumiwa na Tume hiyo.
“Hakuna
ukweli wowote kwamba zile ni mashine za BVR na tumebaini ni feki. Tena
ni sawa na zile zinazotumika kwenye ofisi mbalimbali kuandikisha
wafanyakazi wake. Hao waliosema ni mashine za kuandikisha wapiga kura
hawako sahihi, sio kweli,” alisema Kailima.
Kailima
alieleza kuwa walifanya uchunguzi wa mashine hizo wakiwa pamoja na
baadhi ya viongozi wa vyama vya upinzani vinavyounda Ukawa kwa kuwa wao
ndio waliiopeleka malalamiko kuhusu uwepo wa mashine hizo.
Mashine
hizo zilikamatwa juzi baada ya kuhisiwa kuwa na uhusiano na mashine za
BVR kwa kutokana na mfanano wake na njia zilizokuwa zinatumika
kuwaandikisha wafanyakazi kiwandani hapo. Mashine hizo tayari zilikuwa
zimeandikisha wafanyakazi 100.
Meneja
Mawasiliano wa MM Steel alieleza kuwa mashine hizo zilitumika kwa lengo
la kuandikisha wafanyakazi hao ili kupata taarifa zao kwa lengo la
kupunguza wizi uliokuwa ukifanywa na baadhi ya wafanyakazi na kutokomea.
No comments:
Post a Comment