Uchaguzi wa ubunge jimbo la Arusha Mjini umeahirishwa kutokana na kifo cha mgombea ubunge wa jimbo hilo kwa tiketi ACT-Wazalendo, Estomiah Mallah aliyefariki wakati akipewa matibabu katika hospitali ya rufaa ya KCMC.
Msimamizi
wa uchaguzi jimbo la Arusha, Juma Idd alieleza kuwa walizipokea taarifa
za msiba huo kwa mshituko mkubwa hasa ikizingatiwa kuwa marehemu
aliugua kwa muda mfupi sana.
Msimamizi
huyo alieleza kuwa kufuatia msiba huo, walitoa taaria NEC na hivyo
wamelazimika kuahirisha uchaguzi wa ubunge katika jimbo hilo kwa mujibu
wa sheria ya uchaguzi.
Alifafanua kuwa wananchi jimboni hapo watapiga kura kuchagua rais na diwani pekee.
Alifafanua kuwa wananchi jimboni hapo watapiga kura kuchagua rais na diwani pekee.
Akizungumzia
mazingingira ya kifo cha mgombea huyo, Katibu wa ACT-Wazalendo jimboni
humo, Eliaman Motivo, alisema kuwa wanayo masikitiko makubwa kufuatia
msiba huo kwa kuwa wamempoteza mtu muhimu sana kwenye harakati za
kizalendo za chama hicho na taifa kwa ujumla.
Alisema marehemu alilalamikia hali ya afya yake kwa muda mfupi, lakini hali yake ilibadilika ghafla na kuwa mbaya kabla ya kupoteza maisha.
Alisema marehemu alilalamikia hali ya afya yake kwa muda mfupi, lakini hali yake ilibadilika ghafla na kuwa mbaya kabla ya kupoteza maisha.
“Mzee
alikuwa haumwi lakini kwenye mkutano wa mgombea urais wa chama chetu
Oktoba 6, alipanda jukwaani na baada ya kushuka alisema hajisikii vizuri
na kesho yake ambayo ni Oktoba 7, alikwenda hospitali ya St. Thomas na
alipatiwa matibabu ila hali yake iliendelea kuwa mbaya. Tuliamua
kumhamishia katika hospitali ya rufaa ya KCMC na usiku wa kuamkia jana
alifariki, saa saba,” alisimulia.
Katika
hali ya kusikitisha, katika kampeni za mwaka huu, wagombea watatu wa
nafasi za ubunge wamepoteza maisha. Mgombea wa kwanza alikuwa Mohamed
Mtoi wa Chadema, jimbo la Muheza, mgombea wa pili alikuwa mgombea wa
CCM, Jimbo la Ulanga Mashariki, Bi. Celina Kombani.
Mungu awape faraja familia za marehemu hawa, wapumzike kwa amani. Amina!
No comments:
Post a Comment