Mkutano wa waratibu wa Uchaguzi na wasimamizi wa Uchaguzi kisiwani Pemba - LEKULE

Breaking

6 Oct 2015

Mkutano wa waratibu wa Uchaguzi na wasimamizi wa Uchaguzi kisiwani Pemba


 WASIMAMIZI wa Uchaguzi, Wasimamizi wasaidizi ngazi ya Jimbo Kisiwani Pemba, wakipitia mada mbali mbali zilizotolewa na wakufunzi kutoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Mafunzo hayo yaliyofanyika huko katika ukumbi wa kiwanja cha Makonyo Wawi Chake Chake Pemba.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA.)
 KAIMU mkuu idara ya Uchaguzi kanda ya Zanzibar Bibi Rafiki Kiravu, akiwasilisha mada ya kwa waratibu wa Uchagizi na wasimamizi wa Uchaguzi kisiwani Pemba, huko katika ukumbi wa kiwanda cha Makonyo kisiwani Pemba.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA.)
 MRATIB wa Tume ya Uchaguzi ya Taifa Mohamed Ali Jape, akizungumza na wasimamizi wa Uchaguzi Kisiwani Pemba, huko katika ukumbi wa kiwanda cha Makonyo Kisiwani Pemba.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA.)
 MKUU wa Mkoa wa kusini Pemba Mhe:Mwanajuma Majid Abdalla, akifungua Mkutano wa wasimamizi wa Uchaguzi, waratibu wa Uchaguzi Kisiwani Pemba, huko katika ukumbi wa Kiwanda cha Makonyo Wawi Chake Chake Pemba.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA.)
 WARATIB wa Uchaguzi, Wasimamizi wa Uchaguzi, wasimamizi wasaidizi wa Uchaguzi ngazi ya Majimbo Kisiwani Pemba, wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa kusini Pemba Mhe:Mwanajuma Majid Abdalla, wakati akifungua Mkutano huo katika ukumbi wa kiwanda cha Makonyo Wawi Chake Chake Pemba.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA.)


 AFISA kutoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi Tanzania (NEC)Steven Elisante, akiwasilisha mada ya Taratibu za Upigaji wa Kura kwa wasimamizi wa Uchaguzi, Waratibu na wasimamizi wasaidizi wa Uchaguzi kisiwani Pemba, huko katika Ukumbi wa Kiwanda cha Makonyo wawi Chake Chake Pemba.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA.)
 MMOJA kati ya washiriki wa Mkutano wa wasimamizi wa Uchaguzi Kisiwani Pemba, akiuliza swali katika mafunzo ya wasimamizi wasaidizi wa Uchaguzi kisiwani Pemba.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA.)
MMOJA wa wasimamizi wa Uchaguzi Kisiwani Pemba, akionyesha mmfano wa karatasi ya kupigia kura jinsi inavyotakiwa kukunjwa, wakati wa mafunzo huko katika Ukumbi wa kiwanja cha Makonyo Wawi Chake Chake Pemba.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA.)