Baada ya kuisha kwa zoezi la kupiga Kura lililofanyika leo October 25 2015, najua kila Mtanzania atakuwa na hamu ya kuyapata matokeo.
Lakini zipo taarifa nilizozipata kutoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi NEC ambapo hilo la utaratibu wa utoaji wa Matokeo limeguswa pia >>> “Tumeendesha Uchaguzi wa Rais na Makamu ya Rais, shughuli imeendelea vema… Tumepata taarifa na Zanzibar pia Uchaguzi umeendelea salama.” >>> Ramadhan K.Kailima, Mkurugenzi wa Tume ya Uchaguzi, NEC.
Lakini kuna changamoto pia zilizojitokeza kwenye Uchaguzi huu >>> “Tulipata tatizo kidogo maeneo ya Mkoa wa Rukwa, wakati gari linapeleka vifaa kuna watu waliteka gari, wakalichoma moto na kuharibu vifaa vyote baada ya kutokubaliana na malipo tuliyowapa… Tumekepeleka Karatasi za kupigia Kura kwa ajili ya Kupigia Kura Rais pamoja na Mbunge wa kule lakini Diwani tumeahirisha kwa sababu karatasi zilikuwa chache.”>
“Jeshi la Polisi limekamata watu wote waliohusika na tukio hilo, tumepata tatizo pia maeneo ya Dar es Salaam ikiwemo maeneo ya Kimara watu ndio wanataka kuanza kupiga Kura kwa sababu Karatasi za kupigia Kura ziliharibiwa” >>> Ramadhan Kailima.
Kuna baadhi ya maeneo pia Uchaguzi umechelewa kuanza leo, sababu ni hii hapa >>> “Baadhi ya wadau toka mwaka 2010 walikataa Walimu wasitumike kusimamia Uchaguzi, baadhi ya vijana tuliowachukua kufanya kazi hiyo walifanya uharibifu wa vifaa vyote, imebidi tupeleke vifaa vingine na kazi ya kupiga Kura imeanza japo kwa kuchelewa sana.”
Uchaguzi ukiisha huu ndio utaratibu wa kutolewa kwa matokeo ya Uchaguzi >>> “Matokeo ya awali yataanza kutoka kesho saa tatu asubuhi, tutakuwa tunatoa kwa awamu tatu au nne kwa siku… Itakuwa saa tatu asubuhi, saa sita, saa tisa na saa 12 jioni…”
Na mshindi wa nafasi ya Urais atangazwa kwa utaratibu huu pia >>> “Tarehe 29 saa tatu asubuhi tutamtangaza mshindi wa nafasi ya Urais, tarehe 30 tunamkabidhi Cheti chake halafu tutamkabidhi Serikalini waendelee na shughuli za kumuapisha.” >>>- Ramadhan Kailima.
Sauti yenye taarifa yote hii hapa kutoka Tume ya Uchaguzi NEC.
No comments:
Post a Comment