Gari La Tume Ya Uchaguzi Lazua Utata Kituoni Baada Ya Kukamatwa Likiwa Na Milioni 6 - LEKULE

Breaking

25 Oct 2015

Gari La Tume Ya Uchaguzi Lazua Utata Kituoni Baada Ya Kukamatwa Likiwa Na Milioni 6



Gari lilokodiwa na tume ya uchaguzi ya Wilaya ya Arumeru Mashariki  limezua utata baada ya kukutwa na kiasi cha fedha zaidi ya Sh 6 milioni.

Akizungumzia sakata hilo, Msimamizi Msaidizi wa uchaguzi, kata ya Imbaseny , Jefason Mwangura ,amekiri kubeba fedha hizo kwenye gari hilo mali ya Enong’oto  na kudai kuwa  zilikuwa ni za malipo ya wasaidizi wa vituoni kwa ajili ya kujikimu.

Alisema pia  pesa hizo kwa utaratibu ilikuwa ni kulipa wasaidizi  vituoni ili iweze kuwasaidia kujikimu wakiwa vituoni hapo .

Hata hivyo , Mwangura alisema  Mwenyekiti wa Chadema, kata ya Imbaseny  baada ya kukamata fedha hizo alikimbia nazo kusikofahamika.

“Mimi nashangaa hela zimechukuliwa na aliyechukua amekimbia nazo ,” kama ilikuwa si halali wangezishika wasubiri polisi  ,”alisema Jefason

Mgombea ubunge  wa jimbo la Arumeru Mashariki ,(chadema) Joshua Nasari  alizungumzia tukio hilo na kusema ni kosa kisheria kuzunguka na fedha hizo kwani kisheria ilipaswa zilipwe kabla au baada ya uchaguzi.

No comments: