Kuelekea mechi dhidi ya Simba October 17, Mbeya City imeendelea na mazoezi bila kocha mkuu - LEKULE

Breaking

16 Oct 2015

Kuelekea mechi dhidi ya Simba October 17, Mbeya City imeendelea na mazoezi bila kocha mkuu

Klabu ya Mbeya City ya jijini Mbeya ambayo  October 17 itaikaribisha Simba katika uwanja wa Sokoine Mbeya kucheza mechi yake ya sita ya Ligi Kuu Tanzania bara msimu wa 2015/2016. Mbeya City ambayo inashika nafasi ya 13 baada ya kucheza mechi sita na kushinda moja na kutoka sare moja inashuka uwanjani kucheza ikiwa na huzuni.
IMG-20151016-WA0018
Mbeya City kwa siku za hivi karibuni imeondokewa na aliyekuwa kocha mkuu wa timu hiyo Juma Mwambusi ambaye ameenda kuwa kocha msaidizi wa klabu ya Yanga na kurithi mikoba ya Charles Boniface Mkwasa aliyepata mkataba wa kuwa kocha wa timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars.
IMG-20151016-WA0014
Kwa sasa Mbeya City ina mkosa kocha wake mkuu na nahodha wa klabu hiyo Juma Nyosso ambaye anatumikia adhabu ya kufungiwa kwa kipindi cha miaka miwili, lakini kwa sasa wanafundishwa na kocha wao msaidizi Meja Abdul Mingange bila kuwa na kocha mkuu. Hata hivyo Mbeya City imeendelea na mazoezi ya kuelekea mchezo huo ikiwa na nyota wake kama Juma Kaseja na Haruna Moshi Boban.
IMG-20151016-WA0022
IMG-20151016-WA0020
IMG-20151016-WA0021
IMG-20151016-WA0019
IMG-20151016-WA0015
IMG-20151016-WA0016
IMG-20151016-WA0017
IMG-20151016-WA0013
Boban na Kaseja

No comments: