IMG_6587
Baadhi ya wakazi wa kata ya Kisaki manispaa ya Singida waliohudhuria hafla ya uzinduzi wa mradi wa kufua umeme wa upepo unaotekelezwa na kampuni ya Wind East Africa.
IMG_6596
Makamu wa Rais wa jamhuri ya muungano Tanzania, Dk.Mohammed Ghalib Bilal,akizindua mradi wa kufua umeme wa upepo unaotekelezwa na kampuni ya Wind East Africa katika eneo la kijiji cha Kisaki manispaa ya Singida.

SIKU chache tu baada ya Makamu wa Rais,Dk.Mohamed Gharib Bilali kuweka jiwe la msingi la mradi wa umeme wa upepo katika Kijiji cha Kisaki,Manispaa ya Singida,wananchi jirani wamelalamikia kutolipw afidi na kampuni ya Wind East Africa.
Wananchi waliokusanyika na kulalamika kupitia wawakilishi wao ni kutoka vijiji vya Unyamikumbi “A”,Unyamikumbi “B”,Ughaugha “A”,Ughaugha “B” na Kisaki,vilivyopo kata ya Unyamikumbi na Kisaki.
Wananchio hao wamesema pamoja na kuwekwa kwa jiwe la msingi hawako tayari kuliachia eneo hilo kwa kampuni ya kufua umeme wa upepo ya Wind East Africa kutokana na kampuni hiyo kutoheshimu makubaliano waliyokubaliana na serikali za vijiji hivyo.
Mwenyekiti wa Taasisi za Jumuiya mbalimbali zilizopo katika Kijiji cha Unyamikumbi,Ramadhani Ibrahimu King’wai alisema kwenye kikao cha serikali za vijiji vya Kisaki, Unyamikumbi “A”,Unyamikumbi “B”,Ughaugha “A” na Ughaugha “B” alisema kwamba wanasikitika kw ahatua walioifanya  kampuni hiyo kumuita kiongozi wa kitaifa kuweka jiwe la msingi ilhali wakijua bado hawajamaliza tatizo la fidia.
Akifafanua mwenyekiti huyo alisema uongozi wa kampuni ya Wind East Africa, ofisi ya mkuu wa wilaya  na hata ya mkoa hawakuwatendea haki kumleta kiongozi huyo mkubwa wa kitaifa bila kuwashirikisha wananchi wa maeneo hayo.
Kwa upande wake mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya huduma za jamii wa Kijiji cha Unyamikumbi “B”,Hudu Mohamedi Sunu alibainisha kwamba makubaliano ya uongozi wa kampuni hiyo na wananchi ilikuwa wafanye utafiti kwanza na baada ya kujiridhisha kuwa eneo hilo linawafaa,ndipo wangerudi kukutana na uongozi wa maeneo hayo,kuwekeana mikataba kabla ya kuanza kwa mradi huo.
Akizungumzia mkasa huo, mwenyekiti wa Kijiji cha Unyamikumbi “A”,Juma Hamisi Ngoi aliweka bayana kwamba makubaliano yaliyofikiwa kati ya pande hizo mbili yalikuwa ni baada ya kukamilisha utafiti,walitakiwa kupeleka mrejesho na pia kupeleka ramani inayoonyesha eneo la mradi,kuueleza uongozi wa serikali kuwa mahali ulipo mnara wao ni eneo la Kijiji gani lakini kabla ya kutekeleza makubaliano hayo ndipo ghafla walishitukia ugeni mkubwa wa kitaifa bila wao kushirikishwa katika maandalizi.
“Baada ya jiwe la msingi la mradi huu kuwekwa na kupandwa mti kwenye eneo hilo ambalo hata hawaelewi kamapuni hiyo ilipata maelekezo kutoka kwa nani mwenye eneo hilo kutokana na kufanya shughuli hizo kwa kujiamini kabisa kama vile eneo hilo ni mali yao”.alisema
Alipotakiwa kuzungumzia malalamiko ya wananchi wa vijiji hivyo,mmoja wa wawakilishi wa kampuni hiyo ambaye hakuwa tayari kutaja jina lake kwa kuwa siyo msemaji wa kampuni alikiri kwamba hakuna taarifa iliyotolewa na kampuni hiyo kwenda kwa wananchi hao kuhusu ujio wa Makamu wa Rais.
Aidha aliweka bayana pia kwamba vile vile hakuna mwananchi yeyote aliyepo kwenye eneo la mradi huo anayetakiwa kuondoka kupisha mradi, aliyelipwa fidia na hakuna mrejesho wowote uliotolewa na uongozi wa kampuni hiyo kwa wananchi hao baada ya kufikia makubaliano na Tanesco.
Akizungumza kwa njia ya simu kutoka Dar-es-Salaam,mmoja wa watendaji wa kampuni hiyo,Saidi Abdallah hakuwa tayari kuzungumzia lolote lile zaidi ya kumwambia mwandishi wa habari hizi akaonane na katibu wa mkuu wa Mkoa wa Singida,aliyemtaja kwa jina moja tu la Fuwe.
Katibu huyo alipoulizwa alikiri kufahamu ujio wa makamu wa rais peke yake na maandalizi yalikuwa yakifanywa na uongozi wa kampuni hiyo. Makamu wa Rais Dkt.Bilal amwakilisha Rais Jakaya kuzindua Halotel Tanzania