Mkurugenzi wa
Mipango na Maendeleo ya Biashara, Mhandisi Kato Kabaka (aliyesimama),
kutoka Kampuni ya Uendelezaji Jotoardhi Tanzania akitoa elimu kwa
wananchi wa kata ya Kisaki wilaya ya Morogoro Vijijini namna ya kutafiti
nishati ya Jotoardhi hadi hatua ya kuzalisha umeme na jinsi
itakavyoweza kubadili maisha ya wananchi wa kata hiyo.
Wananchi
wa kata ya Kisaki, Morogoro Vijijini wakimsikiliza kwa makini Bi. Eva
Nyantori, Afisa Sayansi ya Jamii kutoka Kampuni ya Uendelezaji Jotoardhi
Tanzania alipokuwa akiwaelimisha juu ya fursa ambazo watazipata kupitia
mradi wa Jotoardhi.
Afisa
Mawasiliano na Mahusiano ya Umma, Kampuni ya Uendelezaji Jotoardhi
Tanzania Bi. Johary Kachwamba, aliyesimama akiongea na wananchi wa
kijiji cha Kichangani Morogoro Vijijini juu ya mikakati na mipango
ambayo kampuni imejiwekea kuhakikisha megawati 200 za umeme zinalishwa
nchini Tanzania kutokana na nishati ya Jotoardhi ifikapo mwaka 2020.
Mhandisi
wa Mazingira wa Kampuni ya Uendelezaji wa Jotoardhi Tanzania Bi. Esther
Range (aliyesimama) akiwaelimisha wananchi wa kijiji cha Kichangani
namna ambavyo nishati ya umeme wa Jotoardhi ilivyo rafiki wa mazingira
tofauti na nishati nyingine za umeme.
Mwananchi
wa kijiji cha Kichangani Morogoro Vijijini Bwana Hamisi Kadobwa
(aliyesimama) akiuliza swali kuhusu teknolojia ya kuvuna nishati ya
Jotoardhi, aidha ilipongeza juhudi za Serikali kuwaletea wananchi
maendeleo.
No comments:
Post a Comment