Afisa
Mtendaji Mkuu wa Benki ya Posta Tanzania, TPB, Sabasaba Moshingi(wapili
kulia), akihudumia wateja kwenye tawi la benki hiyo Kijitonyama jijini
Dar es Salaam, leo Ijumaa Oktoba 16, 2015, kwenye kilele cha maadhimisho
ya wiki ya huduma kwa wateja ya benki hiyo. (Picha na K-VIS
MEDIA/Khalfan Said)
NA
K-VIS MEDIA
KATIKA
kuhakikisha inatoa huduma bora kwa wateja wake hapa nchini, Benki ya Posta
Tanzania, imeweka mashine maalum ambayo wateja wa benki hiyo wanaofika kupatiwa
huduma watatoa maoni yao juu ya huduma wazipatazo kwa kubonyeza vitufe
vinavyoelekeza nini maoni yake juu ya huduma aliyoipata.
Akizungumza
na waandishi wa habari wakati wa kilele cha maadhimisho ya wiki ya huduma kwa
wateja ya benki hiyo, kwenye tawi lake la Kijitonyama jijini Dar es Salaam,
Oktoba 16, 2015, Aisa Mtendaji Mkuu wa benki hiyo, Sabasaba Moshingi alisema,
benki yake imelenga kutoa huduma zilizo bora na za kisasa ili kurahisisha
utendaji wake wa kazi.
Moshingi
ambaye aliongoza maafisa wa benki hyo kutoka makao makuu kwa kutoa huduma kwa
wateja, kuwasikiliza na kuwasaidia namna ya kujaza fomu na kutoa pesa, alisema,hatua
ya yeye kuongoza maafisa wake kutoa huduma, ni kuwaonyesha wateja kuwa benki
yao inawajali.
“Ili
kufanikisha lengo hili benki imeanzisha matumizi ya mashine za kisasa
zitakazomuwezesha mteja kutoa maoni ya jinsi gani anafurahia au kutofurahia
huduma zetu bila kuhitaji kuandika kwenye karatas, mteja atabofya kitufe ili
kupata maoni yake, nasi tutayafanyia kazi maoni yake haraka iwezekanavyo.”i.”
Alisema Moshingi.
Alisema
matumizi ya mashine hizo yataboresha utoaji huduma za kibenki, na hivi sasa
mipango ya kuziweka kwenye kila tawi inaendelea.
.
Moshingi akimuelekeza mteja namna ya kujaza fomu za kuweka pesa
Afisa wa operesheni wa TPB tawi la Kijitonyama, Agatha Ngoile, (kushoto), akimuhudumia mteja
Mteja akibonyeza kitufe kutoa maoni yake baada ya kupata huduma
Afisa
Mtendaji Mkuu wa TPB, Sabasaba Moshingi, akibadilishana mawazo na
Meneja wa shirika anayeshughulikia mawasiliano, Norvis Moses
Moshingi,
(wapili kushoto), akizungumza na Norvis, huku Meneja wa tawi la TPB,
Kijitonyama, Emmanuel Kimola akiteta jambo na Afisa Habari Theo
Mwakifulefule
Meneja
Masoko wa TPB, Deo Kwiyukwa, (kushoto), Meneja Biashara, Frank Mushi,
(katikati), na Afisa Masoko, Grace Majige, wakibadilishana mawazo
Agatha akiwa kazini
Moshingi akiwa anahudumia mteja kwenye teller
No comments:
Post a Comment