CCM inapenda kutoa taarifa kuhusu masuala kadhaa kwa wanachama, wapenzi na mashabiki wake na kwa umma wa Watanzania.
Kufunga Kampeni
CCM
itafunga kampeni zake kwa utaratibu mpya na kwa kishindo. Kampeni za
CCM zitafungwa kitaifa kwa mikutano mikubwa ya kampeni katika mikoa
mitano. Mikutano hiyo itaongozwa na viongozi wa CCM kitaifa waliopo
madarakani na wastaafu. Mikoa hiyo na viongozi wakaoongoza mikutano hiyo
ni kama ifuatavyo:
1.
Mwanza – Ndugu Jakaya Mrisho Kikwete, Mwenyekiti wa CCM, Dkt. John
Pombe Magufuli, Mgombea Urais, na Ndugu Samia Hassan Suluhu, Mgombea
Makamu wa Rais
2. Tanga – Ndugu Abdulrahman Kinana, Katibu Mkuu wa CCM
3. Mbeya – Ndugu Benjamin William Mkapa, Mwenyekiti wa CCM Mstaafu
4. Mtwara – Ndugu Ali Hassan Mwinyi, Mwenyekiti wa CCM Mstaafu
5. Kigoma – Ndugu Philip Mangula, Makamu Mwenyekiti wa CCM
6. Kilimanjaro – Ndugu Yusuf Makamba, Katibu Mkuu wa CCM Mstaafu
7. Mara – Ndugu Joseph Warioba, Mjumbe wa Kamati Kuu na Waziri Mkuu Mstaafu
Kati
ya leo na kesho, maeneo mengine yanaweza kuongezeka. Mikutano hii
itaanza saa sita mchana na itarushwa, yote kwa pamoja, kwa matangazo ya
moja kwa moja ya vituo vya televisheni vitano na vituoa vya redio 67.
Vilevile, watakaohudhuria katika mikutano hii wataunganishwa moja kwa moja na mkutano wa Mwanza, alipo Mwenyekiti, Mgombea na Mgombea Mwenza, na wataweza kusikiliza hotuba ya Dkt. Magufuli moja kwa moja kupitia screens zitakazokuwa katika viwanjani vyote hivi saba.
Vilevile, watakaohudhuria katika mikutano hii wataunganishwa moja kwa moja na mkutano wa Mwanza, alipo Mwenyekiti, Mgombea na Mgombea Mwenza, na wataweza kusikiliza hotuba ya Dkt. Magufuli moja kwa moja kupitia screens zitakazokuwa katika viwanjani vyote hivi saba.
Namna
hii ya ufungaji wa kampeni itakuwa ni ya kihistoria, na inadhihirisha
nguvu ya CCM inayoiwezesha kufanya mikutano mikubwa ya kampeni kwa siku
moja katika maeneo mbalimbali nchini. Lakini pia tutafanya historia
katika tasnia ya utangazaji wa televisheni hapa nchini kwa kutangaza na
kuunganisha kwa pamoja matukio saba kwa wakati mmoja.
Kwa
upande wa Dar es Salaam, tutafanya mkutano mkubwa wa ufungaji wa
kampeni za Mkoa wa Dar es Salaam, katika Uwanja wa Jangwani, leo,
Ijumaa, tarehe 23 Oktoba 2015.
Siku ya Jumamosi, tarehe 24 Oktoba 2015, Wagombea Ubunge katika majimbo ya Mkoa wa Dar es Salaam watafunga kampeni katika maeneo ya majimbo yao kwa namna mahsusi.
Siku ya Jumamosi, tarehe 24 Oktoba 2015, Wagombea Ubunge katika majimbo ya Mkoa wa Dar es Salaam watafunga kampeni katika maeneo ya majimbo yao kwa namna mahsusi.
Tathmini ya Kampeni
Kama
Chama, tumeridhika na ubora na ukubwa wa kampeni tulizofanya licha ya
changamoto za hapa na pale. Dkt. Magufuli na Ndugu Suluhu wamefanya kazi
kubwa, na kwa bidii kubwa, na maarifa makubwa.
Wamekuwa barabarani kwa siku 57 wakifanya mikutano kati ya 8 hadi 12 kwa siku. Imani yetu ya ushindi inatokana na kazi kubwa waliyofanya. Pia, CCM inawashukuru viongozi, wapenzi wa washabiki wake – wa makundi mbalimbali ya kijamii - kote nchini kwa kazi kwa kazi kubwa ya kampeni waliyoifanya.
Wamekuwa barabarani kwa siku 57 wakifanya mikutano kati ya 8 hadi 12 kwa siku. Imani yetu ya ushindi inatokana na kazi kubwa waliyofanya. Pia, CCM inawashukuru viongozi, wapenzi wa washabiki wake – wa makundi mbalimbali ya kijamii - kote nchini kwa kazi kwa kazi kubwa ya kampeni waliyoifanya.
Kutokana
na kazi kubwa na nzuri iliyofanyika, na kutokana na mwenendo wa tafiti
huru na tafiti zetu za ndani, CCM inategemea ushindi wa asilimia
zisizopungua 69.
Uchaguzi wa Amani
CCM
haitachoka kuendelea kusisitiza uchaguzi wa amani na utulivu. Sisi kama
chama kikubwa cha siasa nchini, chenye wafuasi wengi zaidi, na chenye
dhamana ya uongozi wa dola, tutatimiza wajibu wetu wa kuhimiza utulivu
kwa wapenzi, washabiki na wanachama wetu. Tunawataka na wenzetu wafanye
hivyo.
Kauli
za wenzetu kwamba kura zitaibiwa ni kauli za kutojiamini na kujiandaa
kufanya vurugu. Kauli za kwamba washabiki wa UKAWA wakishapiga kura
wabaki vituoni kulinda kura si kauli za wanaotaka uchaguzi wa amani.
Kwa
utaratibu wetu wa uchaguzi, utaratibu wa pekee kwa Chama kulinda kura
zake ni kwa kupitia wakala wa vyama waliopo kwenye kila kituo cha kupiga
kura na wenye nguvu na mamlaka ya kisheria ya kushuhudia zoezi zima,
kuanzia kupiga kura, kuhesabu kura hadi kutangaza matokeo. Kura
zinapigwa na kuhesabiwa vituoni mbele ya wasimamizi wa uchaguzi,
mawakala wa vyama na waangalizi wa uchaguzi wa ndani na nje ya nchi.
Mawakala
wa vyama na wasimamizi wa uchaguzi wanaweka sahihi kwenye fomu za
matokeo, na matokeo hayo yanatangazwa na kubandikwa kwenye kituo. Kwenye
kituo kikuu cha Tume cha kujumlisha matokeo, mawakala wa vyama pia
huwepo na Tume hujumlisha matokeo kutoka kwenye fomu za matokeo za vituo
vya nchi nzima zilizosainiwa na mawakala wa vyama kwenye kila kituo.
Kwa
viongozi wa UKAWA kuwaambia watu waingie barabarani au kuvizunguka
vituo vya kupigia kura eti ili kulinda kura hakuna maana yoyote zaidi ya
kutafuta namna ya kuhalalisha vujo, vurugu na uporaji na kuwazuia watu
wengine, hasa wanawake, kupiga kura. Tunaviomba vyombo vya ulinzi na
usalama vizuie hili jambo kwasababu halina nia njema.
Mkakati
wa UKAWA ni kufanya vurugu baada ya kushindwa na kutengeneza mazingira
ya mgogoro wa kisiasa ili Jumuiya ya Kimataifa iingilie kati na
kupendekeza kugawana madaraka. Mkakati huo hautafanikiwa. Tunaviomba
vyombo ya ulinzi na usalama vihakikishe ulinzi na usalama wa watu wote
na mali zao siku ya uchaguzi na baada ya uchaguzi.
CCM haitakubali hata kidogo ushindi wake kuhojiwa au kutiliwa shaka kwasababu tu ya vurugu zilizoanzishwa na watu wengine.
Siku
ya Jumamosi, CCM itatangaza namba maalum za simu kwa Watanzania wote
ili siku kabla ya uchaguzi, siku ya uchaguzi na mara baada ya uchaguzi,
waweze kupiga simu au kutuma ujumbe pale watakapokuwa wanabaini au
kushuhudia vitendo vya kuvuruga amani na kuvuruga utaratibu mzima wa
uchaguzi.
Kupokea Matokeo
CCM
imeweka utaratibu wa kupokea matokeo kwa kutumia mawakala wake moja kwa
moja vituoni na kupitia mtandao wa Chama. CCM inategemea kuwa na
matokeo ya uchaguzi nchi nzima ifikapo saa nne usiku, siku ya uchaguzi,
tarehe 25 Oktoba 2015.
Imetolewa na:
January Makamba
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa
Mjumbe wa Kamati ya Kampeni
22 Oktoba 2015.
No comments:
Post a Comment