Watu wapatao 200 wameteketeza kwa moto vifaa vya kupiga kura huku wengine wakiwajeruhi wasimamizi wa uchaguzi kwa kile kinachoonekana kuwa ni hofu ya kusambazwa kwa kura feki.
Katika
tukio lililotokea wilaya ya Sumbawanga, watu hao wanadaiwa kuteketeza
vifaa mbalimbali yakiwamo makasha 45 ya kuhifadhia kura wakidai kuwa
yalikuwa na kura ambazo tayari zilikuwa zimeshapigwa .
Akizungumza
na mwandishi wa habari hizi kwa njia ya simu Kamanda wa Polisi mkoa wa
Rukwa , Jacob Mwaruanda amethibitisha kutokea kwa tukio huo katika
kijiji cha Zimba , Bonde la Ziwa Rukwa wilayani Sumbawanga .
“Niko
njiani nikielekea katika eneo la tukio ni kweli limetokea usiku
wa kuamkia leo ….. vifaa hivyo vilikuwa vikisafirishwa kwenda tarafa
ya Milepa Bonde la Ziwa Rukwa “ alisema
Akisimulia
tukio hilo, Kamanda Mwaruanda alidai kuwa watu wapatao 200 wakiwa na
silaha za jadi yakiwemo mapanga , marungu , mawe na mikuki waliweka
vizuizi vya mawe makubwa barabara kijijini Zimba na kulizuia gari
lililokuwa likisafirisha vifaa hivyo vya kupiga kura kwenda Tarafa
ya Milepa.
Alieleza
kuwa gari hilo lenye namba za usajiri T 865 BEU likiwa na maofisa
wawili wasaidizi wa uchaguzi na dereva lilizuiliwa na watu hao
wenye hasira na kuchoma vifaa vyote vya kupigia kura ambapo watu
wanane wanashikiliwa na Jeshi la Polisi .
Kwa
mujibu wa Mwaruanda hakuna mtu yeyote waliokuwa wakisafiri katika
gari hilo aliyereruhiwa katika tukio hilo ambao majina yao
hayakuweza kufahamika mara moja .
Kwa
upande wake, Msimamizi wa Uchaguzi wa Wilaya ya Sumbawanga , Adam
Missana akizungumza na mwandishi wa habari hizi kwa njia ya simu
amekiri kutokea kwa tukio hilo huo akidai ulitokea katika kijiji cha
Zimba kati ya saa tatu na nne usiku wa kuamkia leo .
Missana
ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Sumbawanga alidai
kuwa watu hao wenye hasira wameteketeza kwa kuchoma moto vifaa
vyote vya kupigia kura zikiwemo karatasi za kupigia kura wagombea wa
urais, ubunge , na udiwani .
“Vifaa
vilivyoteketezwa kwa moto ni pamoja na masanduku ya kuhifadhia
kura yapatayo 45 , taa , kalamu , karatasi za wagombea urais , ubunge
na madiwani “alisisitiza
Akifafanua
aliongeza kuwa baada ya kusambaza vifaa vya kupigia kura katika
Kata ya Zimba walipofika katika kituo cha mwisho ilikiwa tayari ni
saa kumi na mbili jioni askari waliokuwa wakisindikiza gari hilo
waligoma kuendelea na safari kwa madai kuwa wangefika Kata ya Milepa
usiku .
“Hata
hivyo Msimamizi Msaidizi Jimbo, Charles Mwita aliwaasa askari polisi
waendeleee na msafari lakini walikataa hivyo gari hilo
liliendelea na msafari kuelekea Tarafa ya Milepa bila kuwa na ulinzi
wa askari polisi hadi walipo vamiwa na watu hao ambao waliweka
vizuizi vya mawe barabarani kijijini Zimba “ alisisitiza .
Aliongeza
kueleza kuwa gari hilo lilipofika kijijini Zimba watu wenye hasira
walililizua wakiwa na silaha mbalimbali za jadi “walishusha vifaa
vyote vya kupigia kura kutoka garini wakanyonya mafuta kutoka
kwenye gari hilo kisha wakayatumia kuchomea vifaaa hivyo “ alisisitiza
“Maofisa
Wasaidizi wa Uchaguzi wawili na dereva wa gari hilo lililotekwa
wamejeruhiwa na kuporwa simu zao na vitu vingine vya thamani “ alidai Missana .
Kwa
mujibu wa Misaana gari hilo licha ya kuwa na maofisa wasaidizi wa
uchaguzi wawili na wakitoka kwenye mafunzo ambao baada ya gari
hilo kutekwa walifanikiwa kukimbia kusikojulikana .
Alieleza
kuwa baada ya kuwasiliana na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) uchaguzi
utakao fanyika leo katika Kata ya Milepa ni wa Uraisi tu kwa kuwa kwa
taratibu za tume uchaguzi wa Rais hauwezi kuahirishwa .
No comments:
Post a Comment