Mkimbizi
kutoka Burundi,
Philipo Nyandungulu, akishuka kutoka kwenye basi baada ya kuwasili
katika Kambi ya Wakimbizi ya Nyarugusu iliyoko Kasulu Mkoani
Kigoma.Idadi ya Wakimbizi kutoka
Burundi imekuwa ikiongezeka siku hadi siku naWizara ya
Mambo ya Ndani ya Nchi kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa
la
kuhudumiaWakimbizi (UNHRC) imekuwa ikiwahifadhi kwa muda katika kambi
hiyo
Baadhi
ya Wakimbizi kutoka Nchini Burundi,wanaohifadhiwa katika Kambi ya
Wakimbizi ya Nyarugusu iliyoko Wilayani Kasulu Mkoani Kigoma,
wakiwapokea Wakimbizi wenzao (hawapo pichani) waliowasili jana kwa basi
kwa ajili ya kuhifadhiwa katika kambi hiyo.
Mkimbizi
kutoka Burundi, Philipo Nyandugulu (kushoto) na Mkewe Vanisi
Nyandugulu, wakisubiri taratibu za kupangiwa sehemu ya kuishi baada ya
kuwasili katika kambi ya Wakimbizi ya Nyarugusu iliyoko Wilayani Kasulu
Mkoani Kigoma,
baada ya kuwasili katika kambi hiyo jana.
Koplo
Flora Peter wa Kituo cha Polisi katika kambi ya Wakimbizi ya Nyarugusu
akiwa ameshikilia Visu, Panga na Fimbo vilivyokutwa katika baadhi ya
mizigo ya Wakimbizi kutoka Burundi
wanaowasili katika kambi ya Wakimbizi ya Nyarugusu iliyoko Wilayani
Kasulu Mkoani Kigoma. Vifaa vya hatari kama vile visu, panga,
fimbo na mishale haviruhusiwi kumilikiwa na Wakimbizi wapya wanaowasili
Kambini hapo,kwa sababu za kiusalama.
Mkimbizi kutoka Burundi, Nibaruja
Europernce , akihamasisha wenzake wanaowasili katika kambi ya Wakimbizi
ya Nyarugusu iliyoko Wilayani Kasulu Mkoani Kigoma kuhusu taratibu za
kuishi kambini hapo ikiwa ni pamoja na kutekeleza masuala muhimu ya
kiafya,
jana.
Mfanyakazi wa Shirika la Maji na Usafi
wa Mazingira (TWESA)
linalofanya shughuli zake katika kambi ya wakimbizi ya Nyarugusu iliyoko
Wilayani Kasulu Mkoani Kigoma,
Andrea Niyitanga ,Akimnawisha mikono kwa kutumia maji yaliyowekwa dawa,
Mkimbizi kutoka Burundi ikiwa ni mojawapo ya mkakati wakutoa Elimu ya
Afya.
Watoto
wa moja ya familia ya wakimbizi kutoka Burundi
wakielekezwa kuingia katika makazi yao mara baada ya kuwasili katika
kambi ya wakimbizi ya Nyarugusu iliyoko katika Wilaya ya Kasulu Mkoani
Kigoma.
Anayeelekeza ni Mfanyakazi wa Shirika la Maji na Usafi wa Mazingira
(TWESA)
linalofanya shughuli zake katika kambi hiyo.
Wakimbizi kutoka Burundi wakipata
maelezo ya jinsi ya kuishi katika kambi ya wakimbizi ya Nyarugusu
iliyopo Wilayani Kasulu Mkoani Kigoma mara baada ya kuwasili kambini
hapo. Anayetoa maelekezo hayo ni Nayiga Mireye wa Shirika
la Maji na Usafi wa Mazingira (TWESA) linalofanya shughuli zake kambini
hapo.
(Picha zote na Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.)
No comments:
Post a Comment