Wakimbizi: Hungary yafunga mpaka wake - LEKULE

Breaking

15 Sept 2015

Wakimbizi: Hungary yafunga mpaka wake


Familia ya wahamiaji katika kambi kwenye mpaka kati ya Hungary na Serbia, karibu na mji wa Röszke, Septemba 11, 2015.
Familia ya wahamiaji katika kambi kwenye mpaka kati ya Hungary na Serbia, karibu na mji wa Röszke, Septemba 11, 2015.
Na RFI
Wahamiaji wakiangusha kilio mbele ya nyaya walizowekewa ghafla mbele yao: Budapest imefunga Jumatatu mpaka wake na Serbia wakati ambapo nchi za Ulaya zikikutana Brussels, zimekua zikijaribu kutafutia suluhu wimbi la wakimbizi linalotishia uhuru wa kutembea barani Ulaya.
Katika mji wa Röszke, eneo kuu wanakopitia wahamiaji kwenye mpaka wa Serbia, askari polisi kumi na tano wa Hungary wakivalia sare ya bluu wamekua wakiwazuia wakimbizi kupita eneo, wakati ambapo maafisa wengine wakiweka nyaya za kwenye barabara, kwa mujibu wa waandishi wa habari wa AFP.
Wahamiaji waliowasili eneo hilo wakitokea Serbiawamekua wakiangsha walipoona barabara ikifungwa. Na kuanzia siku ya Jumanne wiki hii, Hungary itatekeleza sheria mpya ya kutoruhusu wakimbizi kupitia kwenye mpaka wake.
Wakati huo huo, mjini Brussels, waziri wa mambo ya nje wa Luxembourg, Jean Asselborn, amewaonya viongozi wa Ulaya.
" Kama hatuafikiani kwa pamoja leo, Ulaya itasambaratika ", ameonya Bw Asselborn, ambaye ameongoza kikao dharura cha baraza la mawaziri wa mambo ya ndani wa Umoja wa Ulaya.
Mawaziri hawa waliotafautiana, walikua wakijadili hatua ziliyopendekezwa wiki iliyopita na Tume ya Ulaya, ambayo ilitoa wito kwa Mataifa wanachama kugawana, kwa mujibu wa sheria idadi sawa ya wakimbizi 160,000.

No comments: