Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia CUF, Maalim Seif Sharif Hamad akiwahutubia wananchi wa Tumbe alipotembelea eneo hilo.
Mgombea Urais wa
Zanzibar kupitia chama cha Wananchi CUF, Maalim Seif Sharif Hamad
amewaahidi wakulima wa zao la mwani Zanzibar kuwa atapandisha bei ya zao
hilo mara moja, iwap atachaguliwa kuwa Rais wa Zanzibar katika uchaguzi
mkuu wa mwezi ujao.
Maalim Seif
alisema bei wanayolipwa wakulima ya shilingi 700 na 800 hivi sasa ni
ndogo na hailingani na gharama wanazozitumia wala haiwasaidii wakulima
wengi wao wakiwa ni akinamama katika kuondokana na umasikini.
Mgombea huyo
ambaye pia ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar alisema hayo
alipowatembelea wakulima wa mwani, wakulima wa mpunga na kukagua soko la
mboga mboga na samaki katika majimbo ya Tumbe na Konde, mkoa wa
Kaskazini Pemba.
Awali katika
risala ya wakulima wa mwani na wavuvi wa maeneo hayo iliyosomwa na Aisha
mour Ali walisema wanakabiliwa na tatizo kubwa la ukosefu wa vifaa, bei
isiyoridhisha na kukosa boti za kisasa za kufanyia shughuli za uvuvi.
“Tangu 1994
tulipoanza kulima mwani hatujafaidika na bei tunayo lipya, shilingi 700
tunazopewa hazilingani na ugumu wa kazi hii na hilo tumelilalamikia
miaka mingi”, walisema katika risala hiyo.
Maalim Seif
alisema utafiti uliofanywa unaonesha iwapo wakulima wa mwani
watawezeshwa kutumia mbegu za kisasa na kufanya kazi kitaalamu zaidi,
zao hilo linaweza kutoa mchango mkubwa katika juhudi za kuwatoa wakulima
katika umasikini.
Aliaahidi kuwa
akichaguliwa kuwa Rais wa Zanzibar atahakikisha wanaleta wataalamu wa
kutosha kutoa mafunzo ya uzalishaji bora wa zao hilo, kutafuta vifaa
pamoja na mbinu mbadala kuliongezea thamani za la mwani.
“Azma yangu ni
kuona wakulima wa mwani wananufaika na jasho lao kama vile
wanavyonufaika wakulima wenzao wa zao la karafuu”alisema Maalim Seif.
Aidha, aliahidi
kuwa atahakikisha mwani unaozalishwa Zanzibar una sarifiwa (processing)
kabla a kuuzwa na kuondokana na utaratibu wa kuuzwa mzima, utaratibu
ambao huukosesha thamani kubwa katika soko la Kimataifa.
Kilimo cha zao la
mwanai kimepata umaarufu mkubwa Zanzibar kwa kujumisha wakulima katika
vijiji vya mwambao wa bahari, wengi wao wakiwa ni akina mama, kwa mwaka
wastani wa tani 13, 000 huzalishwa Zanzibar na kuuzwa nje ya nchi.
Kuhusu uvuvi,
Malim Seif alisema azma yake ya siku nyingi ni kuhakikisha wavuvi kote
Zanzibar wanapatiwa vyombo vya kisasa vya uvuvi ambavyo vitawawezesha
kufanya shughuli zao kwa ufanisi mkubwa.
Alieleza kuwa
kinachojitokeza hivi sasa ni kupungua kwa samaki katika eneo la mwambao
wa visiwa, hivyo atahakikisha anaandaa mikakati ya kuwawezesha wavuvi wa
Zanzibar ambao wanafikia 32, 000 kufanya shughuli hizo katika bahari ya
kina kirefu ambapo kuna samaki wa kutosha.
Sambamba na
mikakati hiyo, Maalim Seif alisema atafanya kila njia kuhakikisha zao la
mpunga linazalishwa kisasa chini ya utaratibu wa umwagiliaji maji, kwa
vile mchele ndio chakula kikuu kwa watu wa Zanzibar.
Akizungumza na
wakulima wa mpunga katika mabonde la kinyakuzi na Saninga alisema nia
yake ni kuhakikisha Zanzibar inapunguza utegemezi wa bidhaa za chakula
kutoka nje ya nchi na iweze kuzalisha asilimia 60 ya mahitaji yake ya
chakula hasa mchele.
“Mipango hiyo
itawezekana bila wasi wasi, nitaanzisha benki maaluma ya kusaidia
wakulima, wavuvi na wajasiriamali na wataweas kupata mikopo yenye
masharti nafuu”, aliahidi Maalim Seif.
Aliwataka
watendaji wa Halmshauri ya Wilaya ya Micheweni kutafuta watu wenye uwezo
wa kuliendesha soko jipya la kisasa lililopo katika kijiji cha Tumbe
ili liweze kutumika na kuwanufaisha wakaazi wa maeneo hayo.
No comments:
Post a Comment