Ivan
Matovu akisherehesha harambee ya Childbirth Survival International
iliyofanywa kwa ushirikiano wa Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani siku
ya Jumamosi Septemba 12, 2015 katika chumba cha mkutano cha Nyerere
ndani ya jengo la Ubalozi huo na jumla ya $2,696 zilikusanywa siku hiyo
kwa ajili ya kusaidia kuokoa maisha ya wazazi wanaotarajia kujifungua
katika Hospitali ya Wilaya ya Biharamuro.
CSI
walishawahi toa msaada wa namna hiyo hospitali ya Amana iliyopo Wilaya
ya Ilala jijini Dar na nchini Uganda kwa lengo hilo la kuokoa maisha ya
wazazi watarajiwa wa kujifungua. Takribani ya wazazi 35 hufa kila siku
aidha kwa sababu ya kukosekana vifaa au kwa uzembe na kutokuwepo kwa
elimu ya kutosha itakayosaidia kuokoa maisha ya mzazi hao.
Na
kama ingekua daladala kila siku inatokea ajali na kuua wa 35 nadhani
nchi ingacha shughuli zake na kulitazama swala hilo kwa upana zaidi
lakini mtizamo wa akina mama hao 35 wanaopoteza maisha kila siku kwa
ajili ya kujifungua bado wananchi na serikali haijalichukulia swala hili
uzito unaostahili ya kuokoa maisha ya akina mama hao. PICHA NA
VIJIMAMBO NA KWANZA PRODUCTION
Tausi Swedi mmoja ya waanzilishi
wa CSI akielezea kazi kubwa inayofanywa na Childbirth Survival
International kujaribu kuokoa maisha ya akina mama wanaojifungua.
Mkurugenzi na mmoja ya
waanzilishi wa CSI nchini Tanzania Mama Stella Mpanda akielezea kazi ya
Childbith Survival International nchini Tanzania.
Sandra Kiyonga mmoja wa CSI akielezea jambo.
Jessica Mushala akiipongeza CSI kwa kazi kubwa na nzuri ya kuwasaidia
akina mama wanaojifungua Duniani kote kwa kutoa elimu ya uzazi na vifaa
kwa wazazi na wakunga kujaribu kuokoa maisha ya wazazi wanaojifungua
kutokana na uzembe au kutokua na vifaa ikiwemo elimu ya uzazi.
Kikundi cha utamaduni cha ngoma ya asili aina ya mbuutu ya Uganda ikitumbuiza kwenye harambee hiyo.
No comments:
Post a Comment