VODACOM YAMWAGA VIFAA VYENYE THAMANI YA MIL 4.9 KWA TIMU ZA LIGI KUU (VPL) 2015/2016 - LEKULE

Breaking

3 Sept 2015

VODACOM YAMWAGA VIFAA VYENYE THAMANI YA MIL 4.9 KWA TIMU ZA LIGI KUU (VPL) 2015/2016


Baadhi ya waandishi wa vyombo vya habari mbalimbali nchini wakiwa kwenye hafla fupi ya kukabidhiwa vifaa mbalimbali vyenye thamani ya shilingi milioni 4.9 kwa timu zote zinazoshiriki ligi kuu ya mpira wa miguu ya Vodacom Tanzania bara (VPL) leo vilivyokabidhiwa na mdhamini mkuu wa ligi hiyo kampuni ya Vodacom Tanzania.
Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania, Kelvin Twissa akiongea na waandishi wa habari na wawakilishi wa vilabu mbalimbali wa timu zinazoshiriki ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara, wakati wa hafla fupi ya kukabidhiwa vifaa mbalimbali vyenye thamani ya shilingi milioni 4.9 kwa timu zote zinazoshiriki ligi hiyo leo vilivyokabidhiwa na mdhamini mkuu wa ligi kampuni ya Vodacom Tanzania, kushoto ni Meneja Masoko wa shirikisho la mpira wa miguu Tanzania, (TFF) Peter Simon.
Vijana wakitambulisha jezi mpya za nyumbani na ugenini za timu ya African Sport ya Tanga na vifaa mbalimbali vyenye thamani ya shilingi Milioni 4.9 kwa msimu wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara 2015/2016 zilizokabidhiwa rasmi leo na mdhamini mkuu wa ligi hiyo kampuni ya Vodacom Tanzania.
Wanamitindo  wakipita kuitambulisha jezi mpya za nyumbani na ugenini za timu ya Majimaji na vifaa mbalimbali vyenye thamani ya shilingi Milioni 4.9 kwa msimu wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara 2015/2016 zilizokabidhiwa rasmi leo na mdhamini mkuu wa ligi hiyo kampuni ya Vodacom Tanzania.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa shirikisho la mpira wa miguu Tanzania, Boniface Wambura (kushoto) na Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania, Kelvin Twissa (watano toka kushoto) akiwa kwenye picha na mwakilishi wa timu ya Azam FC pamoja na wanamitindo  waliokuwa wakiitambulisha jezi mpya  za nyumbani na ugenini na vifaa mbalimbali vya timu ya Azam FC  vyenye thamani ya shilingi Milioni 4.9 kwa ajili ya msimu mpya wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara  2015/2016. Vifaa hivyo  vilikabidhiwa leo jijini Dar es Salaam na mdhamini mkuu wa ligi hiyo kampuni ya Vodacom Tanzania.
Boniface Wambura(kushoto) na Kelvin Twissa (watano toka kushoto) akiwa kwenye picha na mwakilishi wa timu ya Coastal Union.
Boniface Wambura(kushoto) na Twissa (watano toka kushoto) akiwa kwenye picha na mwakilishi wa timu ya Mbeya FC pamoja na wanamitindo  waliokuwa wakiitambulisha jezi hizo.
Wambura(kushoto) na Twissa (watano toka kushoto) akiwa kwenye picha na mwakilishi wa timu ya Yanga.
Wambura na Twissa wakiwa kwenye picha ya pamoja na wanamitindo waliokuwa wakizitangaza jezi mpya za timu 16 zitakazoshiriki katika ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara 2015/2016 wakati wa hafla fupi ya kukabidhiwa jezi hizo.
Wambura (kushoto) na Twissa (watano toka kushoto) akiwa kwenye picha na mwakilishi wa timu ya Simba Sports Club.
Kampuni ya mawasiliano ya Vodacom Tanzania, ambayo ni mdhamini mkuu wa Ligi kuu ya mpira wa miguu Tanzania bara leo imekabidhi vifaa kwa timu zinazoshiriki ligi hiyo vyenye thamani ya shilingi milioni 490,000,000/=
Akikabidhi vifaa hivyo leo jijini Dar es Salaam, Mkuu wa Kitengo cha  Masoko na Mawasiliano wa Vodacom Kelvin Twissa,alisema kuwa  kwa mara nyingine tena katika kuhakikisha ligi ya soka nchini inaenda vizuri Vodacom inakabidhi  vifaa mbalimbali vya ligi ambavyo ni jezi mbalimbali, viatu vya mazoezi na mechi, soksi, vilinda ugoko, nguo za mazoezi, nguo za kawaida, gloves na vifaa vingine vingi vinavyohitajika.
“Tunajisikia furaha  kukabidhi vifaa hivi siku ya leo tukiwa tunatekeleza  matakwa ya mkataba wa udhamini, ni imani yetu kwamba timu zitakazoshiriki ligi zimejiandaa vya kutosha kwa msimu mpya wa ligi  wa 2015/2016”Alisema Twissa.
Twissa alisema Vodacom inaendelea kudhamini ligi kuu kwa sababu soka ni mchezo unaopendwa sana hapa nyumbani ukiwa na washabiki wengi hivyo inapenda kuona wananchi ambao baadhi yao ni wateja wake  wanapata burudani ya mchezo waupendao pia siku zote inaamini kuwa michezo ni ajira kubwa duniani kote,ikiendelezwa inaweza kubadilisha maisha ya watu wengi na taifa kunufaika kwa mapato makubwa ya kodi kutoka katika sekta hii.
Aliwataka wadhamini wengine kujitokeza ili kuboresha  zaidi ligi ya Tanzania na kuongeza  maslahi kwa wachezaji wanaoshiriki katika ligi “Tukiunganisha nguvu timu zetu zinaweza kuwa na wachezaji wa kimataifa pia ni muhimu  kwa wadau mbalimbali kuanza kuwekeza katika timu za vijana chipukizi kwa kuwa vipaji vinaanzia ngazi ya chini ambako vinapaswa kuibuliwa na kuendelezwa ”Alisema Twissa.
Naye Ofisa Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi,Boniface Wambura aliishukuru Kampuni ya Vodacom,  na kuvitaka vilabu vinavyoshiriki ligi kuu ya Vodacom kuheshimu chapa ya mdhamini wakati wote wa mechi za ligi.
“Ninatoa mwito kwa vilabu  vyote kutumia jezi zenye nembo ya mdhamini katika kuhakikisha ligi inafanikiwa kama inavyotakiwa,”alisema.
Aliongeza kuwa  TFF isingependa kutumia kanuni na sheria kuadhibu klabu inayokwenda kinyume, bali kila klabu izingatie masharti ya mdhamini  kama ambavyo anavyotimiza haki yake ya kuwapatia vifaa.

Alisema ligi ya mwaka huu itakuwa bora kutokana na maandalizi yote  kukamilika mapema pia timu zitazoshiriki zimeziandaa vya kutosha kuhakikisha ligi inakuwa na msisimko na ushindani mkubwa.

No comments: