Trekta
karibu na mji wa Caen ikielekea katika mji mkuu wa Ufaransa, Paris kwa
ajili ya kushiriki katika maandamano ya wakulima leo Alhamisi Septemba
3, 2015.
Na RFI
Wakulima
wa Ufaransa wana hasira na wamekua wakielezea ghadhabu yao. Wakulima hao
wanatazamiwa Alhamisi wiki hii kuandamana kwa wingi wakiwa na matrekta
yao hadi katika mji mkuu wa nchi hiyo, Paris.
Wakulima
kutoka wilaya 12 watashiriki katika maandamano hayo katika eneo la
taifa. Ujumbe wa wakulima hao utapokelewa leo mchan katika mji wa
Matignon, na mwingine utakwenda Bungeni ili kufikisha malalamiko yake
kwa wabunge. Maandamano haya yenye ushawishi mkubwa yametajwa kuwa ya
kihistoria na wafugaji wengi.
Wakulima
wanaelekea kwanza katika mji wa Paris ili waweze kutambuliwa. Wanahisi
kwamba hawaeleweki na wamekua wakipuuzwa, na raia watambuwe shida na
maisha duni yanayokumba wakulima.
" Kwenda
Paris ni pigo kubwa. Kuna matrekta 1500, kutakuwa na zaidi ya watu elfu 4
hadi elfu 5 mchana huu katika eneo la taifa. hali hii inaonyesha dhiki,
shida ya wakulima. Leo tunahitaji ufumbuzi wa kweli ambao ni endelevu
kwa ajili ya kutupa upya mitazamo na kutupongeza kwa kuamka asubuhi na
kufanya bidhaa bora za kilimo ", amesema Luc Smessaert, makamu wa rais
wa wa Shirikisho la Wakulima nchini Ufaransa (FNSEA).
Viwango
Mzozo huo
pia una sababu zaidi ya kiuchumi na kijamii. Bila shaka, wakulima hawa
hawategemei kitu cha ajaabu, lakini wanataka ufumbuzi katika madai yao.
Miongoni mwa madai yao, wanaiomba serikali punguzo la gharama ya kazi
wanaoifanya na gharama za wafanyakazi. Hizo ni moja ya pointi muhimu.
Ufaransa
inaendesha shughuli hii ya kiliomo kwa viwango wakati majirani zake,
Ujerumani na Hispania huzalisha kwa nafu na kuuza zaidi nje.
"
Serikali inapaswa kujitoa kwa kimuundo, na kutupunguzia mzigo wa gharama
na kutupunguzia pia viwango vya ilivyoweka. Na kusema kwamba nafasi kwa
Ufaransa ni kuwa na mifugo yenye maziwa, ng'ombe na nguruwe ",
amesisitiza Thierry Roquefeuil, rais wa Shirikisho la kitaifa la
Uzalishaji wa Maziwa.
No comments:
Post a Comment