NTAGANDA ANAKANUSHA MASHTAKA YANAYOMKABILI-ICC - LEKULE

Breaking

3 Sept 2015

NTAGANDA ANAKANUSHA MASHTAKA YANAYOMKABILI-ICC


Aliyekuwa kiongozi wa waasi nchini Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Bosco Ntaganda

Aliyekuwa kiongozi wa waasi nchini Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Bosco Ntaganda amekanusha mashtaka yaliyokuwa yakimkabili ya uhalifu wa kivita na ukatili dhidi ya binadamu, baada ya kufikishwa katika mahakama ya Kimataifa ya makosa ya jinai, ICC, iliyoko mjini tThe Haque.
Bosco Ntaganda anatuhumiwa na mashtaka 18 ikiwemo kuhusika na mauaji ya zaidi ya raia 400, kuwabaka watoto waliokuwa wamesajiliwa jeshini kama watumwa wa ngono na kupanga na kuendesha kampeini ya kikatili Mashariki mwa Congo. Mashtaka yote yanahusiana na wakati alipokuwa akiongoza mapigano katika eneo la Ituri Mashariki mwa Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo mwaka wa 2002 na 2003.
Watoto waliokuwa wamesajiliwa jeshini.

Ntaganda anatarajiwa kukutana ana kwa ana na baadhi ya watu walioadhirika wakati waa vita hivyo.
Baada ya miaka kadhaa ya mapigano, Ntaganda alijisalimisha mwaka wa 2013, katika ubalozi wa Marekani nchini Rwanda na kutaka kuwasilishwa kwa mahakama ya ICC.
Ntaganda alijulikana na The Terminator na watu wengi humtambua kutokana na jinsi anavyolinda ndevu zake na kofia kubwa kubwa na jinsi anavyopenda maisha ya starehe.
Awali Bensouda alimtaja Bosco Ntaganda kama mtu mwenye sifa mbaya. Bensouda amesema Ntaganda aliwalazimisha mamia ya watoto kujiunga na jeshi lake na kwamba wanajeshi wasichana walibakwa na kuwekwa kama watumwa wa ngono.
Wakili wa Ntaganda anayetoka Canada, aliambia wanahabari kuwa tangu atupwe korokoroni, Ntaganda amepunguza sana uzani wake na anawakosa watoto wake 7.
Lakini kiongozi huyo wa zamani wa kundi la waasi, anasubiri sana kujitetea kwa kutoa hotuba kortini.
Zaidi ya waathiriwa 2000 wameidhinishwa kushiriki katika kesi hiyo kama mashahidi.
Upande wa mashtaka unapanga kuita wanajeshi watoto wa zamani kama mashahidi katika kesi hiyo.
Kiongozi huyo wa mashtaka alisifu Congo kwa ushirikiano wake na ICC na kutoa wito kwa waathiriwa wawe na subira, akisema, lengo moja muhimu la haki ni kufichua ukweli.

NA BBC SWAHILI

No comments: