Mshereheshaji
wa mkutano huo Prof. Venant Nantulya akiwa katika hatua ya uendeshaji
wa mkutano wa Viongozi wa ngazi ya juu wa dini katika kupambana na
kuweka mikakati ya kuharakisha kumaliza maambukizi mapya ya
VVU/UKIMWI.(Picha na Geofrey Adroph).
Mufti
mkuu wa Zambia, Sheikh Assadullah Mwale akifungua kwa dua katika
mkutano wa viongozi wa dini wa nchi za mashariki na kusini mwa Afrika
uliofanyika jana jijini Dar.
Bi. Vanessa Anyoti kutoka
YWCA Tanzania (kushoto) akizungumza kuhusiana masuala ya kijinsia
pamoja na maendeleo ambayo yanaweza kupunguza maambukuzi ya Virusi vya
UKIMWI. Kulia ni Mkuu wa ofisi na mwakilishi wa Shirika la Umoja wa
Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni, Bi. Zulmira Rodrigues.
Mwenyekiti
wa Mtandao wa Kimataifa wa viongozi wa dini waishio na VVU/UKIMWI na
waliyoathiriwa na UKIMWI (INERELA+) Mch. Mpumzile Mabizela akizungumza
na Viongozi wa ngazi ya juu wa dini na wawakilishi wa madhehebu ya dini
kutoka nchi 17 za Mashariki na Kusini mwa Afrika wakati wa mkutano
ulioanza jana jijini Dar.
Mkuu
wa ofisi na mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi
na Utamaduni, Bi. Zulmira Rodrigues akisoma hotuba kwa Viongozi wa
ngazi ya juu wa dini na wawakirishi wa dini waliofika kwenye mkutano
uliofanyika jijini Dar es Salaam, Tanzania kujadili na kuweka mikakati
ya kuharakisha kumalizama ambukizi mapya ya VVU/UKIMWI.
Dk.Warren
Namara kutoka shirika la (UNAIDS) akielezea ni kwa njia gani viongozi
wa kidini wanaweza kuelimisha jamii inayowazunguka jinsi ya kupambana na
kuepuka maambukizi mapya ya virusi vya UKIMWI.
Mwenyekiti
wa Tume ya kudhibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS), Dk. Fatma Mrisho akitoa
wito kwa mashirika mbalimbali kujikita katika utoaji wa elimu kuhusu
maambukizi ya virusi vya UKIMWI huku wakishirikiana na Viongozi wa ngazi
ya juu wa dini.
Baadhi
ya Viongozi wa ngazi ya juu wa dini na wawakilishi wa madhehebu ya dini
kutoka nchi 17 za Mashariki na Kusini mwa Afrika wakiwa kwenye mkutano
huo utakaodumu kwa takribani siku tatu.
Picha ya Pamoja Kwa washiriki walio hudhuria mkutano huo.
Na Mwandishi wetu
Viongozi
wa ngazi ya juu wa dini na wawakilishi wa madhehebu ya dini kutoka nchi
17 za Mashariki na Kusini mwa Afrika wakutana Dar es Salaam, Tanzania
kujadili na kuweka mikakati ya kuharakisha kumaliza maambukizi mapya ya
VVU/UKIMWI Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni
(UNESCO) kwa kushirikiana na Mtandao wa kimataifa wa Viongozi wa dini
wanaoishi na virusi vya UKIMWI (INERELA+) pamoja na Shirika la Umoja wa
Mataifa linaloshughulikia masuala ya UKIMWI (UNAIDS) waandaa mkutano wa
siku tatu wa kimataifa kujadili ushiriki wa taasisi na viongozi wa dini
katika kukabiliana na maambukizi mapya ya VVU/UKIMWI.
Mkutano
huo ulioanza jana tarehe 02/09/2015 unafanyika katika hotel ya
Kunduchi, Dar es Salaam, Tanzania na unaohudhuliwa na zaidi ya viongozi
50 wangazi ya juu wa dini na wawakirishi wamtandao wa INERELA kutoka
nchi 17 za Mashariki naKusini mwa Afrika ikiwemo Tanzania.
Wengine
wanaohudhuria mkutano huo ni wawakirishi wa makundi ya vijana;
wawakilishi wa mashirika ya umoja wa mataifa na wawakilishi wataasisi za
serikali ikiwemoTume ya Taifa ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania na UNESCO
Tanzania.
Katika
mkutano huo Mwenyekiti wa Mtandao wa Kimataifa wa viongozi wa dini
waishio na VVU/UKIMWI na waliyoathiriwa na UKIMWI (INERELA+) Mch.
Mpumzile Mabizela ameeleza umuhimu wa kiongozi wa dini na namna kiongozi
wa dini anavyoweza kushiriki katika kutoa elimu kuhusu maambukizi ya
UKIMWI, matumizi sahihi ya dawa zakupunguza makali ya VVU, unyanyapaa na
namna watu wanavyoweza kujikinga na maambukizi kupitia semina
mbalimbali zinazokuwa zikiendelea katika Misikiti na madhehebu
mbalimbali.
Kwa
upande wake Mkuu wa ofisi na mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa
la Elimu, Sayansi na Utamaduni, Bi. Zulmira Rodrigues amewataka viongozi
wa dini kujikita katika jamii kwa ajiri ya kutoa elimu inayohusu Virusi
vya UKIMWI hususani kwa vijana na jamii iliyopo vijijini.
Aliongeza
kuwa kutokana na sababu za kiutamaduni na mira wazazi wengi wanashindwa
kuongea na watoto juu ya masuala ya jinsia, balehe na mahusiano
inachangia vijana wengi kukosa elimu sahihi juu ya miili yao hususani
afya ya uzazi na kujikuta wanapata matatizo ikiwemo mimba za utotoni na
maambukizi ya VVU.
Akisistiza
umuhimu wa viongozi wa dini katika mapambano dhidi ya UKIMWI na mimba
za utotoni, Bi. Zulmira Rodrigues aliwataka viongozi hao kushirikiki
kamirifu katika kutoa elimu sahihi na kujiepusha na ushauri
utakaowasaidia waamini na vijana “wakati dunia inategemea mchango wenu
katika kuhakikisha watu wanazingatia matumizi sahihi ya dawa, baadhi
yenu m mekuwa mkitoa elimu zinazochangia watukuacha matumizi ya dawa na
hatimaye kuathiri kinga zao za mwili” alisema. Bi. Zulmira na kugusia
suala la unyanyapaa na namna viongozi wa dini wanavyoweza kusaidia
kupunguza“msiwatenge na kuwanyanyapaa watu wanaoishi na Virusi vya
UKIMWI kwani wanahitaji elimu zaidi ili waweze kuwa katika hali ya
kawaida nasi ya kiunyonge”alisema.
Naye
Mwenyekitiwa Tume ya kudhibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS) Dk. Fatma
Mrisho alitoa wito kwa mashirika mbalimbali kusaidiana na viongozi wa
kidini katika kuhakikisha watu wana hamasika na kupima afya zao kila
wakati na kusambaza elimu inayohusu maambukizi ya Virusi vya UKIMWI kwa
maeneo mbalimbali na pia awaasa vijana ambao bado ni wadogo
kutokujiingiza katika ulimwengu wa ndoa kwani vitendo hivyo vinachangia
kwa kasi maambukizi mapya ya VVU.
Kwa
upande wake Dk.Warren Namara kutoka shirika la (UNAIDS), aliongeza
kuwa viongozi wa dini ni viongozi waaminifu waadilifu na ni
waelimishaji.
Kulingana
na huduma yao ya kukutana na waumini kila wiki wana nafasi nzuri na pia
ni rahisi sana kuweza kuwafikishia ujumbe na kuwahamasisha wananchi
katika maeneo yao kwa kutoa elimu ya virusi vya UKIMWI. Dk Warren
alisisitiza haki ya kila mtu kupata elimu sahihi na kuwataka viongozi wa
dini kutowatenga watu hasa walio kwenye hatari zaidi ya kupata
maambukizi mfano watu wanaotumia madawa ya kulevya na watu wanaofanya
biashara ya kuuza miili yao.
No comments:
Post a Comment