DSC01622
Meneja wa benki ya Posta tawi la Singida, Redenoter Rweyemamu, akizungumza kwenye hafla ya benki hiyo kutoa msaada wa shuka 104 yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni mbili, kwa hospitali ya mkoa mjini hapa, inayokabiliwa na uhaba wa shuka na kusababisha wagonjwa kutumia mashuka yao binafsi kitendo ambacho ni kinyume na taratibu.
DSC01626
Mganga mfawidhi wa hospitali ya mkoa mjini hapa, Dk. Daniel Tarimo, akitoa shukrani zake kwa benki ya posta tawi la Singida mjini kwa msaada wake wa mashuka kwa hospitali hiyo.Dk.Tarimo amedai kuwa bado hospitali hiyo inaupungufu wa shuka 2,000 na magodoro 236.
DSC01611
Meneja wa benki ya Posta tawi la Singida mjini (katikati),akimkabidhi Mganga mfawidhi wa hospitali ya mkoa mjini hapa, Dk.Daniel Tarimo mashuka 104. Mashuka hayo yamepunguza makali ya uhaba mkubwa wa shuka na sasa, kuna upungufu wa shuka 2,000 na magodoro 236.
DSC01629
Bango la benki ya posta.(Picha na Nathaniel Limu).

Na Nathaniel Limu, Singida
BENKI  ya Posta Tawi la Singida Mjni, imetoa msaada wa shuka 104 yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni mbili kwa hospitali ya mkoa ya mjini hapa, ili kupunguza uhaba mkubwa unaoikabili hospitali hiyo.
Akizungumza kwenye hafla ya kukabidhi msaada huo, Redempter Rywemamu, alisema hatua hiyo imechukuliwa  na benki ya posta,ikiwa ni  ni kuitikia  wito uliotolewa na mkuu wa mkoa wa Singida Dk. Parseko Kone, kusaidia hospitali hiyo shuka, kwa lengo la kumaliza tatizo linaloelekea kuwa sugu la uhaba wa shuka.
“Sisi kama benki ya posta, tunalo jukumu la kuhakikisha tunashiriki kikamilifu kutatua kero zinazoikabili jamii ambayo ndani yake, hapo wateja wetu. Hospitali yetu hii ya mkoa, tunafahamu inapokea wagonjwa na majeruhi wengi, kwa hiyo pamoja na msaada wa leo, niahidi tu kwamba tunaendelea kusaidia kadri uwezo utakavyoturuhu” alisema.
Naye Afisa muuguzi wa hospitali hiyo, Amina Mlangida, alitumia fursa hiyo kuishukuru benki ya Posta Singida, kwa msaada wa mashukua hay, kwa kudai msaada huo umetolewa kwa wakati muafaka.
Alisema hospitali hiyo kongwe mkoani hapa, inakabiliwa na uhaba mkubwa wa shuka unaochangia wagonjwa kutumia mashuka yao binafsi, kitendo ambacho ni kinyume na taratibu.
“Afisa Mlangida alitumia nafasi  hiyo kuwaomba  wadau wengine wa sekta ya afya, kuiga mfano wa benki ya Posta, katika kusaidia kupunguza uhaba mkubwa  wa shuka kwenye hospitali hii ya Mkoa”,alisema.
Kwa upande wake, Mganga mfawidhi wa hospitali ya mkoa mjini hapa, Dk. Daniel Doniel Tarimo, alisema baada ya kupokea msaada wa mashuka kutoka benki ya Posta, bado hospitali hiyo inakabiliwa na uhaba wa mashuka 2000, magodoro 236.
Dk. Tarimo alitumia fursa hiyo kuialika benki ya posta kwa ajili ya kukutana  na wafanyakazi wa hospitali hiyo,  ili kuwafahamisha/kuwaelemisha juu ya  huduma zinatolewa na benki hiyo, pamoja na mikopo itakayosaidia kupunguza makali ya maisha ya wafanyakazi hao.