Zipo nchi Duniani ambazo huwa hazipendezwi na aina ya hukumu ambazo zinatolewa na China hasa kwa watu waliokamatwa kwa makosa ya jinai kama ya ubadhirifu ama ishu ya kukamatwa na dawa za kulevya, lakini kwa upande mwingine hukumu za aina hiyo zimesaidia kuwatia hofu watu kujiingiza na kufanya makosa ya aina hiyo.
Dar es Salaam ni moja ya Majiji ambayo kiukweli hali ya usafi na utunzaji wa Mazingira sio ya kuridhisha kwenye maeneo mengi, lakini kuna Miji kama Moshi wameweza kujitahidi kutokana na adhabu kali ambayo imewekwa ikitokea umekamatwa kwa kosa la uchafuzi wa Mazingira, faini yake tu inaogopwa !!
Ripoti kutoka China inaonesha kwa kipindi cha miezi saba ndani ya mwaka 2015,wamekusanya Yuan Milioni 28 zilizotokana na faini kwa kesi za Uchafuzi wa mazingira…Hizo ni zaidi ya Trilioni 9 kwa pesa ya Tanzania !!
Kilichofanyika ni kwamba January 2015 walifanya marekebisho ya Sheria ambapo kuanzia hapo Kiwanda au mtu yoyote akikamatwa kwa kosa linalohusu uchafuzi wa mazingira faini yake ni kubwa na hakuna kiwango cha mwisho ambacho mtu anatakiwa kulipia.
Pesa iliyokusanywa China kwa miezi saba tu ni karibia nusu ya Bajeti ya Tanzania 2015-16, ikitokea Dar au Tanzania kunakuwa na Sheria kali kiasi hicho unadhani tutamaliza tatizo la uchafu
No comments:
Post a Comment