Majibu ya Roma Mkatoliki baada ya single yake mpya kuzuiliwa kuchezwa kwenye vituo mbalimbali - LEKULE

10 Sept 2015

Majibu ya Roma Mkatoliki baada ya single yake mpya kuzuiliwa kuchezwa kwenye vituo mbalimbali


.
.
Kazi yangu ni kuhakikisha nakusogezea kila stori inayonifikia na hapa ninayo stori iliyochukua headlines Sept 9,2015 ya msanii wa Hip Hop kutokea 96.0 (Tanga) Roma Mkatoliki ambaye single yake mpya ilizuiliwa kwenye baadhi ya vituo vya radio nchini.
Msanii huyo alipokutana na ripota wa millardayo.com aliweza kuelezea sababu zilizopelekea kuzuiliwa kwa single yake mpya iitwayo Viva Roma na kusema..’Kiukweli jana ndio ilikuwa tarehe 9 mwezi wa tisa ambayo nilitoa ahadi kwa watu kuwa nitaachia wimbo wangu mpya unaoitwa Viva Roma na asubuhi mapema kabisa kwenye ukurasa wangu wa instagram nilipost picha ikionesha napaki CD zangu nikiwa tayari kuisambaza kazi yangu mpya mimi na timu yangu nzima ya Tongwe Records; – Roma Mkatoliki
.
.
‘Ilikuwa saa saba nianze na Eatv Radio kwenye kipindi cha Planet Bongo, saa nane nitaenda XXL ya Clouds FM, halafu nitaenda Times FM, halafu nitaenda E FM, na Magic FM so nilikuwa natoa ratiba ya kuitambulisha wimbo wangu katika vituo mbalimbali vya radio’ – Roma Mkatoliki
‘Ila mpaka sasa tunavyoongea tumeshaisambaza katika vituo vyote mbalimbali sehemu ambayo bado ni kwenye mitandao tu kama blogs, website na nchi za jirani ila jibu nililopewa na baadhi ya vituo vya radio ni kwamba wameikataa kuicheza ngoma yangu kwasababu wanachodai kwamba ina maneno makali huku vituo vingine vikiwa vinacheza verse moja tu kiukweli imenisikitisha lakini kwa upande wa mashabiki wanasema wimbo ni mzuri na sio kama ninalaumu vituo vya radio ila ndio maamuzi yao – Roma Mkatoliki

No comments: