Meneja wa
Program wa Haki Elimu,Godfrey Bonaventura akizungumza na waandishi wa
habari juu ya utafiti uliofanywa na International Budget Partinership
leo jijini Dar es Salaam,Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Haki Elimu,John
Kalage
Mkurugenzi
Mtendaji wa Haki Elimu, John Kalage akizungumza na waandishi wa habari
leo wakati wa utoaji wa Uwazi wa Bajeti katika utafiti uliofanywa na
Interntional Budget Partinaship iliyofanyika leo jijini Dar es
Salaam.kushoto ni Meneja Program wa Haki Elimu, Godfrey Boneventura
(picha na Chalila Kibuda Globu ya Jamii)
Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii
TANZANIA imekuwa ya tatu katika nchi za Afrika Mashariki katika uwazi bajeti kwa wananchi kwa kupata alama 46.
Utafiti
huu umefanywa kwenye nchi 142 ambazo zimesaini kuingia katika uwazi wa
bajeti kwa wananchi ambazo hufanyika kila baada ya miaka miwili.
Akizungumza
na waandishi wa habari Meneja wa Programu wa Haki Elimu,Godfrey
Bonavetura amesema kutokana na Tanzania kupata alama 46 inatakiwa kutoa
taarifa za bajeti kwa wakati.
Nchi ya
Uganda nidio inayoongoza katika uwazi wa bajeti kwa kuwa na alama
ikifuatiwa na Kenya kwa kuwa na alama 48 hali ambayo inafanya Tanzania
kuongeza kasi katika uwazi wa utoaji bajeti.
Amesema
Tanzania ni nchi ya tatu kutokana na kutoa taarifa chache za bajeti na
kutoa mara kwa mara inaondoa ufisadi kwani wananchi wana kuwa uaminifu
wa serikali wa serikali yao kutokana na taarifa zinazopatikana katika
bajeti.
No comments:
Post a Comment