Ofisa
Habari wa Kituo cha Redio cha EFM, Samira Sadiq (kushoto), akizungumza
na wanahabari (hawapo pichani), kabla ya kumkaribisha Meneja wa
Mawasiliano wa redio hiyo kuzungumza na waandishi wa habari kuhusu
tamasha la muziki mnene bar kwa bar litakaloanza kesho kutwa Jumamosi,
Agosti 5, 2015 Mkuranga mkoani Pwani. Kulia ni Meneja Usambazaji na
Mauzo wa Kampuni ya Simu ya Smart, Haidari Chamshama na katikati ni
Meneja wa Mawasiliano wa EFM Redio, Denis Ssebo. Kampuni ya simu ya
Smart wamedhamini tamasha hilo.
Meneja
wa Mawasiliano wa EFM Redio, Denis Ssebo (kushoto), akizungumza katika
mkutano huo. Kulia ni Meneja Usambazaji na Mauzo wa Kampuni ya Simu ya
Smart, Haidari Chamshama.
Meneja Usambazaji na Mauzo wa Kampuni ya Simu ya Smart, Haidari Chamshama (kulia), akizungumza kwenye mkutano huo.
Mkutano na wanahabari ukiendelea.
Meneja
wa Mawasiliano wa EFM Redio, Denis Ssebo (kushoto), na Meneja
Usambazaji na Mauzo wa Kampuni ya Simu ya Smart, Haidari Chamshama,
wakiwaonesha moja ya jezi zilizotolewa na kampuni hiyo kwa ajili ya
tamasha hilo.
Wanahabari kutoka vyombo mbalimbali wakiwa kwenye mkutano huo kuchukua taarifa hiyo.
Dotto Mwaibale
TAMASHA
la Muziki Mnene Baa kwa Baa linatarajia kuanza kufanyika jumamosi ya
Septemba 5, mwaka huu, wilayani Mkuranga mkoani Pwani.
Akizungumza
na waandishi wa habari Dar es Salaam leo asubuhi, Meneja wa Mawasiliano
wa Kituo cha Redio cha EFM, Denis Ssebo alisema kuanza kwa tamasha hilo
kesho ni baada ya kumalizika kwa Tamasha la musiku mnene Mtaa kwa Mtaa
awamu ya kwanza, (Muziki mnene bango) ambapo mashabiki na wasikilizaji
wengi wa EFM wameweza kujishindia zawadi kabambe, Sasa ni zamu ya
wapenzi wa burudani na mambo ya party.
Ssebo
amesema Muziki mnene bar kwa bar ni tukio ambalo lina wakutanisha
wasikilizaji na mashabiki wa EFM na wakali wa EFM kutoka wilaya za
kinondoni, Ilala na Temeke katika mkoa wa Dar er Salaam, na sasa
wameamua kuupekea katika mkoa wa Pwani.
Ametaja
maeneo ambayo wanatakiwa kukaa tayari kwa Muziki mnene bar kwa bar
utakaoporomoshwa na Rdjs wakali wa Efm, ni pamoja na Kibaha, Mlandizi,
Mkuranga, Bagamoyo, Kisarawe,
Kigamboni na maeneo mengine mengi kwa ajili ya kuhakikisha tunakonga nyoyo za mashabiki wetu.
Ameongeza
kuwa Muziki Mnene bar kwa bar mwaka huu utaanza rasmi kesho jumamosi
Mkuranga ambako mbali na kutoa Burudani, wataanza na mchezo wa mpira ili
kuwapa nafasi wale wasio na uwezo wa kujumuika nasi tuonane nao
mchana.
Ssebo
amesema mwishoni watafanya Tamasha kubwa la hitimisho ambalo
litafanyika jijini Dar es salaam ambalo safari hii limeboreshwa na
kuongezwa vionjo vingi sana.
“Ninawaomba wasikilizaji wetu wakae mkao wa kula maana
tutawafikia na kuwamiminia burudani ambayo pia itarushwa live
kutoka eneo husika kupitia kituo chao cha 93.7 EFM. Njoo
tuonane, tufahamiane na tuijenge Radio yetu efm ambayo kwetu
Muziki unaongea”.
Muziki
mnene awamu hii umedhaminiwa na kampuni ya simu mpya kabisa hapa
Tanzania ya Smart, kampuni ambayo huduma zake ni za gharama ndogo
zaidi, kwa hiyo mwaka huu Smart watakuwa na sisi katika kuupeleka
Muziki Mnene bar kwa bar kwa mashabiki wa EFM.
Dotto Mwaibale
TAMASHA la Muziki Mnene Baa kwa Baa linatarajia kuanza kufanyika jumamosi ya Septemba 5, mwaka huu, wilayani Mkuranga mkoani Pwani.
Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo asubuhi, Meneja wa Mawasiliano wa Kituo cha Redio cha EFM, Denis Ssebo alisema kuanza kwa tamasha hilo kesho ni baada ya kumalizika kwa Tamasha la musiku mnene Mtaa kwa Mtaa awamu ya kwanza, (Muziki mnene bango) ambapo mashabiki na wasikilizaji wengi wa EFM wameweza kujishindia zawadi kabambe, Sasa ni zamu ya wapenzi wa burudani na mambo ya party.
Ssebo amesema Muziki mnene bar kwa bar ni tukio ambalo lina wakutanisha wasikilizaji na mashabiki wa EFM na wakali wa EFM kutoka wilaya za kinondoni, Ilala na Temeke katika mkoa wa Dar er Salaam, na sasa wameamua kuupekea katika mkoa wa Pwani.
Ametaja maeneo ambayo wanatakiwa kukaa tayari kwa Muziki mnene bar kwa bar utakaoporomoshwa na Rdjs wakali wa Efm, ni pamoja na Kibaha, Mlandizi, Mkuranga, Bagamoyo, Kisarawe,
Kigamboni na maeneo mengine mengi kwa ajili ya kuhakikisha tunakonga nyoyo za mashabiki wetu.
Ameongeza kuwa Muziki Mnene bar kwa bar mwaka huu utaanza rasmi kesho jumamosi Mkuranga ambako mbali na kutoa Burudani, wataanza na mchezo wa mpira ili kuwapa nafasi wale wasio na uwezo wa kujumuika nasi tuonane nao mchana.
Ssebo amesema mwishoni watafanya Tamasha kubwa la hitimisho ambalo litafanyika jijini Dar es salaam ambalo safari hii limeboreshwa na kuongezwa vionjo vingi sana.
“Ninawaomba wasikilizaji wetu wakae mkao wa kula maana
tutawafikia na kuwamiminia burudani ambayo pia itarushwa live
kutoka eneo husika kupitia kituo chao cha 93.7 EFM. Njoo
tuonane, tufahamiane na tuijenge Radio yetu efm ambayo kwetu
Muziki unaongea”.
Muziki mnene awamu hii umedhaminiwa na kampuni ya simu mpya kabisa hapa Tanzania ya Smart, kampuni ambayo huduma zake ni za gharama ndogo zaidi, kwa hiyo mwaka huu Smart watakuwa na sisi katika kuupeleka Muziki Mnene bar kwa bar kwa mashabiki wa EFM.
No comments:
Post a Comment