Wanaume wa shoka wakilisakata rhumba wakati wa kuwafurahisha mashabiki wa bendi ya Skylight wakati wa mkesha wa eid 
Mwimbaji wa bendi ya Skylght Natasha akiwa anawapa mashabiki vionjo vya nyimbo za taratibu (kistaarabu) wakati wa mkesha huo wa Eid ndani ya kiwanja cha Escape One Mikocheni
Bendi ya waimbaji wakali wa Skylight ikirindimisha baadhi ya nyimbo zao huku mbele kabisa akiwa anawaongoza wenzake katika uimbaji wa nyimbo hiyo Sony Samba.
Ashura Kitenge (kushoto) akiwa na Kasongo Junior wa Skylight band wakitoa burudani ya kukata na shoka kwa mashabiki wao ndani ya kiwanja cha Escape One Mikocheni
Sam Mapenzi ni muimbaji mashuhuri na huwa anajua kukonga nyoyo za watu hususani katika ule muziki wa Afrika magharibi weee utampenda hata kwa mkopo, hapo akiwa anaimba kwa kushirikiana na wenzake ndani ya bendi ya Skylight siku ya mkesha wa Eid.
Baadhi ya waimbaji wa bend ya Skylight wakitoa burudani kwa mashabiki wao usiku wa kuamkia  sikukuu ya Eid.
Hii siku zote huwa inapatikana ndani ya Skylight tu na sio kwingineko maana ukihitaji kuburudika njoo tuungane pamoja katika bendi yetu inayoenda kwa kusikiliza mashabiki zaidi na sio kubagua mashabiki.
DSC_0237
Ile kauli ya mteja ni mfalme inadhihirika hapa wakati mashabiki wameamua kuungana na waimbaji wa bendi yao ya Skylight ili kuhakikisha mambo yote yanaenda sawa kiburudani zaidi.
Kwa style tofauti tofauti fika uungane na Skylight band ili uweke shida pembeni na kuweza kufurahia maisha ni kila siku ya Jumapili tukutane ndani ya Escape One Mikocheni kukonga nyoyo zetu na Skylight band
Mashabiki sasa zamu yao kulisakata wakati bendi ya Skylight ikiwa inatoa burudani hiyo ndani ya Escape One Mikocheni
Rapa mkongwe kwenye muziki wa Live Joniko Flower akiwa katika hatua yake ya kukusanya mashabiki ili tu waende sawa aisee huyu jamaa ni hatari jumapili hii atakuwepo pale Escape One Mikocheni bila kukosa sogea taratibu uje ushuhudie vitu kutoka Skylight band.
Sony Masamba mwenye nguo nyeupe wa kwanza ambaye ni muimbaji wa bendi ya Skylight akienda sawa na mashabiki wa bendi hiyo kwa kulisakata rumba

mashabiki wa bendi ya Skylight wakiserebuka kwa raha zao wenyewe fika na wewe ili upate burudani ya kukata na shoka.
Kasongo Junior akitoa burudani ya kuwaimbia mashabiki wa bendi ya Skylight kwani yeye ni mtaalamu wa sauti yenye mvuto mkubwa ambapo huto tamani kukosa kumsikiliza kila aingiapo jukwaani.
Sam Mapenzi akiwa katika ishara ya kuimba kwa hisia ndani ya viwanja vya Escape One Mikocheni kwenye mkesha wa Eid
ukafika ule wakati wa shock dance hapo sasa fika jumapili hii ili upate vitu hatari kutoka Skylight band
New style ya nyimbo yao ni pamoja na hii hapa wakiwa wameweka mkono mmoja kwa hewa ,Skylight band Wazee wa style mpaka wewe mwenyewe useme basi
Sam Mapenzi (kushoto) akiwa na Ashura Kitenge wakitoa burudani ya nguvu ndani ya Skylight band wakati wa mkesha wa kuamkia sikukuu ya Eid
Vijana wa Skylight band hao katika ubora wao fika uone jinsi wanavyo kupeleka katika mapumziko ya fikra zako.
Mmoja wa viongozi wa Bendi ya Skylight Joshua Ndege (katikati) akionyesha umahiri wake sambamba na waimbaji wa bendi hiyo.
Kushoto Rapa mkongwe katika  muziki wa Live Joniko Flower pamoja na mwenzake Sony Masamba wakisababisha mashabiki viuno vyao viweze kuzungushwa mithiri ya feni.