1
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake waliotaka kujua jinsi alivyoshughulikia migogoro ya Ardhi nchini.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi amekutana na wananchi wa Dar es salaam wenye Migogoro ya Ardhi na kufanikiwa kupokea Malalamiko yao Katika mkutano wa siku mbili wa tarehe 22 na 23, Septemba, 2015 katika Makao Makuu ya Wizara ya Ardhi. Wananchi wengi waliofika katika mkutano huo walisifu jitihada za Waziri Lukuvi katika kushughulikia Migogoro ya Ardhi ambapo tarehe 22 Septemba 2015 alipokea Malalamiko ya Wananchi kwa Manispaa ya Kinondoni na tarehe 23 Septemba 2015 alipokea Malalamiko ya Wananchi kwa Manispaa ya Temeke na Ilala.
2
Waziri wa Ardhi Mhe. William Lukuvi pamoja na Naibu wake Mhe. Angela Kairuki wakipokea malalamiko ya wananchi wenye migogoro ya ardhi katika mkoa wa Dar es salaam.
3
Waziri wa Ardhi akimsikiliza kwa makini mwananchi mwenye malalamiko ya mgogoro wa ardhi kutoka manispaa ya Kinondoni.
4
Baadhi ya Wananchi wa Dar es salaam wenye Migogoro ya Ardhi wakiwa katika mkutano huo.(Picha na KITENGO CHA MAWASILIWANO SERIKALINI WIZARA YA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI).