Viongozi wakuu wa umoja wa katiba ya wananachi UKAWA wakiongozwa na mwenyekiti wa chama cha Democrasia na maendeleo CHADEMA Mh FREMAN MBOWE pamoja na makamu mwenyekiti wa CHADEMA Profesa SAFARI na kaimu mwenyekiti wa chama cha wananchi CUF ambaye pia ni mbunge wa bunge la Africa mashariki Mh TWALHA TASLIMA jana jioni walihudhuria Baraza la kuu la idd lililoamndaliwa na Taasisi za kiislam Tanzania, shughuli iliyofanyika katika hotel ya LAMADA Jijini Dar es salaam.
Katika
shughuli hiyo ambayo iliambatana na dua mbalimbali pamoja na hotuba za
viongozi mbalimbali pia walialikwa wagombea urais wa vyama vyote
Tanzania lakini hakuna hata mmoja aliyeweza kufika huku mgombea wa UKAWA
akiwakilishwa na Mh FREMAN MBOWE.
Mh
mbowe alipata nafasi ya kutoa Hotuba fupi ambayo iliwagusa mamia ya
waislam ambao walikuwa katika shughuli hiyo na hapa nimekunukulia baadhi
ya mambo ambayo mbowe aliyazungumza na kushtua wengi
Baadhi ya mambo aliyoongea Mh Freeman Mbowe
1-Nashukuru
sana kwa ukaribisho wa shughuli hi,mgombea wetu ndugu EDWARD LOWASA
alitamani kuwa nasi jioni hii lakini kutokana na ratiba ya kampeni
kubana imebidi aunganishe kwenda kwenye kampeni za kesho huko manyara
2-Swala
la mashekh ambao wapo jela bila hukumu yoyote,tulisema siku ya ufunguzi
wa kampeni na tunaendelea kusema kuwa tumewaagiza wanasheria wa chama
chetu kufwatilia kwa makini na kuona nini hasa kimetokea kwao kama kuna
mahali kunahitajika msaada wa kisheria tupo tayari kulishuhulikia hilo
kwani sisi lengo letu ni kurudisha umoja na mshikamano Tanzania.
3-Zimebaki siku takribani 30 sasa kabla ya watanzania kufanya maamuzi halisi,ni muda wa maamuzi ndugu watanzania.
4-TANESCO
imefilisika na watanzania wengi hawajui hili,sasa shirika la umeme
halina hata sent na wameamua kufanya mgao wa kimya kimya lakini ukweli
ni kwamba huu mgao ni mkubwa sana huko tuendako kwa sababu hawana hela
na wanaficha ukweli,kuna mgao mkali sana sasa wa kimya kimya na
utaendelea kuwa mkali kadiri siku zinavyokwenda.
5-Kuna
wizi mkubwa sana wa mafuta Tanzania na kuna baadhi ya watu wakubwa
wanauratibu wizi huo,Tanzania ina akiba ya mafuta hadi mwezi wa 11
lakini serikali imetoa hati ya kuingiza mafuta nchini ambapo baadhi ya
wahusika ni familia ya Rais KIKWETE.
6-Serikali
yetu ya awamu ya tano sio serikali ya visasi kama inavyodhaniwa,ila ni
serikali ya kuwarudisha watanzania pamoja kwa maridhiano,na
maelewano,ila kuna watu itabidi washughulikiwe kwa mijibu wa sheria
kutokana na kuligharimu taifa hao tutafanya hivyo.
7-Tume
ya uchaguzi ya miezi miwili iliyopita sio tume ya sasa,mwenyekiti yupo
ila watendaji wengi wameondolewa bila sababu za msingi.
8-Mtendaji
mmoja mkuu wa tume juzi tumepata taarifa kuwa ameondolewa na kupelekwa
kusikojulikana na amerudhishwa na kutakiwa kukabidhi ofisi mara moja.
9-Tume
ya sasa inaongozwa na wanajeshi na usalama wa taifa,mimi mbowe ndio
nasema kama kuna mtu anabisha waje wanikamate leo,hatuwezi kuvumiliana
kiasi hiki ni wakati wa kuwekana wazi ili watanzania wafanye jambo
wanalolitaka.
10-Nasema hivi hatutakubai hujuma hizi ambazo zinaendelea sasa tutasema hadi mwisho.
11-Mwisho
kabisa nasema hivi ni wajibu wetu kutafuta kura,kupiga kura na kulinda
kura hivyo ndugu zangu waislam nawaomba tushirikiane katika hili,
ASANTENI KWA KUNISIKILIZA