Afisa
Mtendji Mkuu wa Shaer illusions mama Shekha Nasser Akiwaeleza jambo
washiriki wa Semina ya Ujasiriamlai ( hawapo pichani) Namna ya
Kujitangaza kwa Kutumia njia mbalimbali , kuwahudumia na kuwajali
wateja wao.Semina hiyo iliyo chini ya Manjano Foundation ina lengo la
kuwajengea uwezo wana wake kujikita kwenye biashara hasa kwa kutumia
Vipodozi vya Luv Touch Manjano anayeshuhudia ni Mkufunzi wa Maswala ya Biashara Ndugu Felix Maganjila.
Baadhi ya washiriki wakisikiliza kwa makini mada Mbalimbali zinazojadiliwa kwenye semina hiyo.
Mafunzo
ya Ujasiriamali Phase II ya Wanawake kupitia Vipodozi vya LuvTouch
Manjano yameingia siku ya tatu leo ambapo Mkufunzi wa Maswala ya
Biashara Ndugu Felix Maganjila ametoa mada kuhusu namna ya kutafuta
wateja na njia mbalimbali za kuuza bidhaa.Washiriki walipata nafasi ya
kwenda kutafuta masoko (Marketing Research) maeneo tofauti ya Jiji la
Dar es salaam pamoja na kuangalia changamoto kubwa za namna ya kuuza
bidhaa zao kwa wateja wa Luvtouch na namna bora ya kuwashawishi wakazi
wengine kutumia kipodozi pendwa cha LuvTouch Manjano.
Mkufunzi wa Maswala ya Biashara Ndugu Felix Maganjila Akieleza jambo namna ya Kuendesha biashara kwa washiriki hao .
Waliweza
kuwaelezea wateja wapya kuhusu ubora wake pia kuwa wazalendo na kuunga
kwa kutumia bidhaa za LuvTouch ambayo ni bidhaa ya kwanza na ya pekee
ambayo ni Make-up brand ya Kitanzania inayozalishwa na Shear illusions
inayomilikiwa na mzalendo mama Shekha Nasser. Baadhi ya washiriki
waliopata fursa ya kufanya mauzo maeneo mbalimbali walifanikiwa kuuza
bidhaa za LuvTouch Manjano.
Kwa
Upande wa Afisa Mtendji Mkuu wa Shaer illusions mama Shekha Nasser
amewataka washiriki wanapoanzisha biashara zao na kujikota katika tasnia
ya vipodozi ni muhimi hao kujitangaza ipasavyo kwa kutumia njia
mbalimbali za bei nafuu maana bila matangazo hakuna biashara.
Washiri wa semina hiyo wakifurahiya jambo
No comments:
Post a Comment