Radio 5 Arusha – wasaka wasanii wenye vipaji mtaani jijini Dar - LEKULE

Breaking

14 Sept 2015

Radio 5 Arusha – wasaka wasanii wenye vipaji mtaani jijini Dar


????????????????????????????????????
Wasanii wenye vipaji vya kuimba wakihakiki majina yao kwa DJ Haazu, wa Radio 5 wakati wa mchakato wa RADIO 5 KAMATA KIPAJI uliofanyika katika viwanja vya TP SINZA Jijini Dar es salaam Septemba 12, 2015.wenye lengo la kusaka vijana wenye vipaji na kuwainua kutokana na vipaji vyao.(PICHA ZOTE NA PHILEMON ).
Katika kuonyesha kuwa wapo karibu na vijana wa Kitanzania katika kuwasaidia kuwainua kiuchumi na kiuwezo,kituo cha Radio maarufu kutoka kaskazini mwa Tanzania ARUSHA Radio 5 kimenzisha mchakato maalum wa kusaka vipaji kwa vijana wa kitanzania mchakato ambao umeanzia Jijini Dar es salaam ukiwa na lengo la kuhakikisha kuwa wanamuwezesha kijana mwenye kipaji kufikia malengo na ndoto zake.
3
DJ Haazu akiwajibika.
Radio 5 imekuwa na michakato mbalimbali ili kusaidia vijana katika secta tofauti tofauti zinazohusu maisha yao ya kiuchumi huku ikiwa inawaunga mkono vijana wenye shughuli mbalimbali ambao hufika radioni hapo kuomba sapoti ikiwa ni pamoja na vijana wa sarakasi, ujasiriamali na fani nyingine.
Mchakato ambao sasa unatajwa kuwa utakuwa msaada mkubwa kwa vijana ambao umezinduliwa Jijini Dar es salaam na kupewa jina la ‘RADIO 5 KAMATA KIPAJI’ katika viwanja vya TP Sinza darajani ilishuhudiwa vijana wengi wakijitokeza kuonyesha vipaji vyao ili waweze kuibuka na zawadi mbalimbali ambazo zinatolewa na waandaji hao.
2
Wafanyakazi wa RADIO 5 wakishangilia wakati Wasanii mbalimbali ambao ni vijana wenye vipaji wakati wakionesha vipaji vyao jukwaaji (kulia), Mtangazaji wa Redio 5 Mwangaza Jumanne (katikati), Meneja masoko na mawasiliano Sarah Keiya na kushoto ni Meneja Vipindi, Mathew Philip.
Katika zoezi hilo vijana walitakiwa kutuma nyimbo zao radioni ikiwa ni pamoja na kujiandikisha majina yao ili siku waandaaji hao watakapofika katika mtaa waliopo basi waweze kupata nafasi ya kuonyesha vipaji vyao,na kupatikana washindi ambapo mchakato huo utapita katika maeneo yote ya jiji la Dar es salaam na mwisho kuwapata washindi wanne ambao ndio watakaoibuka na zawadi kabambe.
Lengo kuu la mchakato huo ni kuwasaka vijana ambao wanavipaji na wapo mtaani kutokana na sababu mbalimbali ambazo wameshindwa kuonyesha vipaji hivyo ambapo RADIO 5 wameamua kupita katika mitaa hiyo kuhakikisha kuwa vijana hao wanapata nafasi ya kuonyesha vipaji walivyo navyo kwa watanzania.
16
Umati wa mashabiki waliojitokeza kushuhudia wasanii wenye vipaji jukwaani.
Wakati zoezi hilo likiendelea mtandao huu ulipata nafasi ya kuzngumza na Mkurugenzi wa RADIO 5, Bw ROBERT FRANCIS ambaye amesema kuwa ni jambo jema kuona kazi hilo imeanza kwa amani na furaha hivyo watanzania waendelee kuwaunga mkono huku akiwataka vijana mbalimbali wenye vipaji mkoani Dar es salaam kuendelea kujitokeza maeneo mbalimbali ambapo ziezi hilo litakuwa linafanyika pamoja na kuendelea kusikiliza Radio hiyo.
Naye Meneja vipindi wa RADIO 5 Ndugu MATHEW PHILIP akizungumza na mtaandao huu wakati zoezi hilo likiendelea amesema kuwa kupitia vipindi vya Radio hiyo hasa vipindi vya kutafuta vipaji nyumba kwa nyumba Dar es salaam vijana wataweza kuinua vipato vyao huku akisisitiza kuwa watanzania waendelee kusikiliza RADIO 5 kwani kuna mambo mengi na mazuri yanaendelea kuwajia.
4
Msanii akilimiki jukwaa.
Meneja biashara wa kituo hicho cha Radio Bi ANGELA MAINA alisema kuwa maana halisi ya kufanya zoezi hilo ni kuwapa vijana nafasi ili kukuza vipaji vyao hasa katika tasnia ya music ili miaka ijayo watanzania waone matunda ya kazi hiyo haswa kwa washiriki wa zoezi hilo.
Aidha Meneja masoko na mahusiano wa RADIO 5, Bi SARAH LAZARO alisema kuwa pamoja na lengo kuu la mchakato huo ni kuvumbua na kunyanyua vipaji lakini pia ni nafasi kwa wadau wa biashara na mashirika binafsi haswa yanayojihusisha na maswala ya kijamii kuanza sasa kushirikiana na radio 5 ili kukuza biashara zao na kushiriki katika kuendeleza jamii.
5
Mtangazaji wa kituo hicho Julius Kamafa.
Katika mchakato huo endelevu utakaofanyika katika jiji la Dar es salaam unatarajia kuwapata washindi wanne wa mkoa huu ambapo washindi hao watajinyakulia zawadi mbalimbali kama ifuatavyo
Mshindi wa kwanza anataraji zawadi ya kurekodi albam nzima bure kwenye studio za kisasa na kupata promotion kubwa ya kazi yake, mshindi wa pili anataraji kurekodi nyimbo mbili bure pamoja na promotion ya miezi sita(6), mshindi wa tatu atapata kurekodi nyimbo moja pamoja na promotion ya miezi mitatu, huku mshindi wanne ataweza kurekodi nyimbo moja pamoja na promotion ya mwezi mmoja.
6
Msanii Hance Mpozi kutoka Tegeta Dar es Salaam akionesha kipaji chake.
7
Mashabiki.
9
Wasanii wa kundi moja wakimiliki jukwaa.
10
Ni Msaga Sumu akitoa burudani.DSC_0166
Mtalamu wa kiduku.
11
14
12
DSC_0180
Kulia ni DJ Haazu, pamoja na wasanii.
15
????????????????????????????????????
20
Wafanyakazi wa Redio 5 wakiwa katika picha ya pamoja.

No comments: