KATIBU wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, amesema kadi za chama hicho alizokabidhiwa Mgombea wa urais kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Edward Lowassa akiwa Jimbo la Mtama si za kweli, bali mpango uliotengenezwa ili wajipatie umaarufu.
Nape
alisema hayo wakati akizungunza na mwandishi mjini Morogoro juzi mara
baada ya uzinduzi wa safari ya wasanii wanaounda kundi la NimEs’tuka
Hapa kazi tu, linaloongozwa na Aunty Ezekiel na Vincent Kigosi ‘Ray’
uzinduzi uliofanyika kwenye Uwanja wa Shule ya Msingi Kiwanja cha Ndege
Manispaa ya Morogoro.
Septemba
23, mwaka huu wakati wa mkutano wa kampeni za Mgombea wa urais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chadema, Lowassa katika kundi la
vyama vinne vinavyounda Ukawa ambapo pamoja na mambo mengine, ilidaiwa
kadi 3,000 za cha CCM zilipokewa kutoka kwa wanachama na kuunga mkono
Ukawa.
Kwa
mujibu wa Nape, wakati kadi hizo zinapokelewa na Waziri Mkuu mstaafu
aliyehamia Ukawa, Frederick Sumaye, yeye hakuwepo jimboni, bali alikuwa
katika shughuli za kampeni za chama chake nje ya mkoa.
“Kadi
zote waliozipokea ilitokana na kutengeneza shoo, zote zilikuwa ni mpya
hakuna hata moja ya zamani, kwa maana ni mpango mzima wa kutengeneza
shoo na Sumaye ndiye alizipokea si mgombea wa urais wa Chadema,” alisema Nape na kuongeza:
“Hii yote inamaanisha kuwa wananiogopa, binafsi sikuwepo...nilikuwa kwenye kampeni kwa wagombea wa chama changu .”
“Hii yote inamaanisha kuwa wananiogopa, binafsi sikuwepo...nilikuwa kwenye kampeni kwa wagombea wa chama changu .”
Kuhusu
uzinduzi huo, alisema wasanii hao ni miongoni mwa waliorejea CCM kutoka
Ukawa, watazunguka nchi nzima na watapita kila kona ya Tanzania
kuwaambia wananchi na vijana nini walichoona wakiwa Ukawa.
Naye
Aunty Ezekiel akizungumza mbele ya umati wa wananchi waliokuwepo
uwanjani hapo, alisema Ukawa hali si nzuri na kwamba alichambua mchele
na pumba ndiyo maana ameamua kurudi CCM.
Alisema
mgombea wa urais wa Ukawa, Lowassa amekuwa akihubiri kutaka mabadiliko
bila kazi tofauti na mgombea wa urais wa CCM ambaye anahimiza kufanya
kazi.
Naye Kigosi ‘Ray’ alisema ameamua kurudi CCM baada ya kuona kuna vitu ambavyo hawavipati kule Ukawa ambavyo vipo ndani ya CCM na alichokiona kikubwa ni siasa za hadaa tupu ‘magumashi.’
Naye Kigosi ‘Ray’ alisema ameamua kurudi CCM baada ya kuona kuna vitu ambavyo hawavipati kule Ukawa ambavyo vipo ndani ya CCM na alichokiona kikubwa ni siasa za hadaa tupu ‘magumashi.’