MWENYEKITI wa Jumuiya ya Wazazi CCM Taifa, Abdallah Bulembo amepiga marufuku uwanja wa jumuiya hiyo uliopo eneo la Milango Kumi wilayani Kahama mkoani Shinyanga kutumika kwa mikutano ya kampeni za siasa kwa vyama vinavyounda umoja wa Ukawa kwani uwanja huo ni rasilimali ya wanaCCM.
Bulembo
alitoa onyo hilo mwishoni mwa wiki iliyopita wakati alipomkaribisha
Mgombea urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk John Magufuli aliyefika
kwa wakazi wa Mji wa Kahama kwa lengo la kuomba kura.
Alimtaka
Dk Magufuli autumie uwanja huo vyema kuomba kura kwani ni wake kwa kuwa
baadaye ndiye atakayekuwa Mwenyekiti wa CCM Taifa pindi
atakapochaguliwa.
Alimweleza mgombea urais mbele ya wananchi kuwa uwanja huo ni mali ya wanaCCM kupitia Wazazi ambao ndio wamiliki na wameuweka mahususi kwa kuandaa mikakati ya ujenzi wa Chuo cha Ufundi katika eneo hilo, hivyo uwanja huo usitumike kwa siasa na vyama pinzani badala yake CCM pekee wataendelea kuutumia.

“Mambo
yakiwa mazuri hapa tulipo watajenga shule ya ufundi ‘Veta,’ uwanja huu
Chadema hawaruhusiwi kufanya mikutano ya kampeni za siasa ya Ukawa hapa,
siyo eneo lao, tusiwaone hapa watafanya mikutano ya kampeni za CCM
pekee.”
Pia
Bulembo aliwaeleza wananchi hao kuwa Ukawa kuongoza nchi ni ndoto kwani
Mgombea urais kwa tiketi ya CCM amefanikisha kupiga mikutano mingi huku
akisema mikutano rasmi kwa siku moja ni 110 isiyo kuwa rasmi ni 420, na
kutembea umbali wa kilometa 15,600 kwa siku kitu ambacho wao hawana
uwezo nacho.