Mjumbe wa Kamati ya Ushindi ya Chama Cha Mapinduzi, Nape Nnauye ametumia dakika takribani 10 kumshambulia mgombea urais kwa kiketi ya Chadema, Edward Lowassa aliyewahi kuwa kada wa chama hicho.
Nape
alirusha makombora yake kwa Lowassa jana alipopewa nafasi ya kumnadi
mgombea urais wa CCM, Dk. John Magufuli katika viwanja vya Samora, mjini
Iringa.
Alisema
Lowassa ni mwizi na fisadi na kwamba hakuna sehemu ambayo alipewa
kufanya kazi katika ngazi za CCM na serikali bila kuiba.
Nape
alidai kuwa Lowassa alishindwa kukaa katika chama cha
Mapinduzi kwa kuwa hawezi kufugika...."Lowassa ni
Kunguru,Hafugiki." Alisema Nape.
Katika
hatua nyingine,Nape alidai kuwa Lowassa aliwanunua viongozi wa
ngazi za juu wa UKAWA na CHADEMA ili apate nafasi ya
kugombea kupitia Chadema ambayo awali ilikuwa ikimuita fisadi.
Katika
maelezo yake,Nape alisema mbunge wa Iringa mjini,mchungaji Peter
Msigwa ni miongoni mwa walionunuliwa na Lowassa kwa shilingi
milioni 340.
Nape
amekuwa akirusha makombora kwa Lowassa tangu alipotangaza
uamuzi wake wa kukihama chama hicho na kujiunga CHADEMA.
Nape
aliwahi kunukuliwa akisema kuwa amekuwa akipambana na Lowassa
kwa miaka 12 ndani ya CCM na kwamba mziki wake anaufahamu
Hata hivyo, tangu alipoanza kampeni zake,Lowassa amekuwa kimya bila kujibu mashambulizi ya Nape na viongozi wengine wa CCM,hali inayomfanya azidi kujipatia umaarufu mkubwa zaidi wa kiasiasa.
Wakati Nape akitumia muda mrefu kurusha makombora, Lowassa yeye alikuwa Jijini Tanga akifanya mkutano mkubwa wa kampeni uliolazimika kukatishwa kutokana na mafuriko ya wananchi kuzidi eneo la mkutano.
Tazama Video Hapo Chini Kumsikiliza Nape